LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 16, 2024

ZIARA YA DK NCHIMBI KURINDIMA MBEYA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapimduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye Leo anamalizia ziara yake mkoani Songwe, baadaye jioni anatinga mkoani Mbeya kwa kufanya mkutano wake wa hadhara katika Mji wa Mbalizi.

Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea leo katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
0754264203

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages