LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 29, 2024

SG MSIGWA AZINDUA ALBUM YA 'BILA CHANZO HALISI HUTOBOI', ATOA HABARI NJEMA YA KUPONA KICHWA PAPOHAPO BAADA MAOMBEZI YA BABA HALISI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Mlimani City
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema Serikali inalipongeza Kanisa Halisi kwa  kuwalea wananchi vizuri, kusimamia imani na kushirikiana na jamii na serikali katika kuimarisha huduma za jamii.

Amesema hayo, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Albamu ya 'Bila Chanzo Halisi Hutoboi' II ya Waibaji wa Sauti Moja wa Kanisa hilo, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, jana Aprili 28, 2024.

"Kwa niaba ya serikali naomba kulipongeza Kanisa Halisi kwa kuwalea wananchi vizuri, linasimamia imani, linashirikiana na jamii na serikali katika kuimarisha huduma za jamii.

Mimi nafahamu ambavyo Kanisa hili limekuwa likitoa mchango mkubwa kwa jamii tangu lilipoanzishwa hadi leo. Nikiwa Ikulu nimeshuhudia namna ambavyo lilisaidia katika utatuzi wa  changamoto ya watoto wetu kukaa chini madarasani na mengine mengi yaliyofuata baadaye", alisema Katibu Mkuu Msigwa na kuongeza;

"Nataka kuwahakikishia kwamba serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa hili katika masuala yote yanayohusu maendeleo, imani, upendo, kwa sababu dunia inapita kwenye changamoto ya watu kukosa upendo. Ukisikia wanauana, vita, fitina na kuharibiana ni kwa sababu upendo unatoweka na Kanisa Halisi limeamua kusimamia upendo. Tupo pamoja.

Nchi yetu na nchi nyingi za Afrika zinapita kwenye changamoto ya vita vya uchumi. Vita vya uchumi dawa yake siyo kupiga maneno, dawa yake siyo uchawi, dawa yake ni kufanya kazi. Na Kanisa Halisi limeamua kusimamia ajenda ya uzalishaji.

Baba Halisi tunakushukuru sana. Kwa lugha za vijana nataka kuwaambia vijana wote tukae humo, vijana tukitaka kutoboa tukazalishe, bila kuzalisha, uende kwa mganga, ucheze kamari, ulalamike, huendi kokote, ukitaka utoboe lazima uzalishe, hakuna mbadala".

Katibu Mkuu Msigwa akatoa mfano akisema, "Mnayeniona hapa nimetoka katika familia masikini, baba yangu na mama yangu hawajui kusoma wala kuandika, nilikuwa nikienda shuleni kwa kutoroka shambani, hapa nilipofika ni kwa sababu ya bidii ya kufanya kazi", kisha akasema;

"Baba Halisi umesema jambo zuri kwamba kwenye makubaliano na Kanisa, ni marufuku mtu kuzurura Kanisani bila kazi, kwamba tunapokwenda Kanisani tunaenda kumshukuru Mungu lakini Ibada yetu ni kazini,  yaani Kama Baba Halisi alivyosema twende kazini tukamshukuru Mungu lakini Ibada tukaifanyie Kazini.

Hili jambo la kuhimiza  kila mtu kufanya kazi, tukilisimamia vizuri hii nchi tatuitwa masikini. Unaitwaje masikini, una mikono, miguu, una Baba Halisi anakuombea, kuwa Masikini haiwezekani. kuishi kwa  uzalishaji na kuishi kwa upendo inawezekana.

Manzoni mwa hotuba yake, Katibu Mkuu Msigwa alitoa habari njema (ushuhuda), akisema, "...nimefika hapa kichwa kikiwa kinauma sana, lakini baada ya maombezi ya Baba Halisi hivi sasa hakiumi, kimepona".

Mapema, akimkaribisha Katibu Mkuu Msigwa, Baba Halisi alimtambulisha kuwa Kanisa Halisi misingi ya Kanisa Halisi ni Amani, Upendo usiobagua, Kuzalisha kwa haki, yaani kipato anachopata mtu kiwe cha haki, na kwamba kwenda nyumba ya Ibada ni kwa ajili ya kumshukuru Muumba kwa kumwezesha kufanya kazi kwa haki na kwamba kufanya kazi yoyote kwa haki ndiyo Ibada.

Pia Baba Halisi alimwambia Msigwa kwamba Msimamo wa Kanisa Halisi hawajihusishi na siasa lakini kila alfajiri huwaombea viongozi ili waweze kutongozwa wananchi vizuri, na wakikuta unamsema vibaya mwanasiasa unaombewa.

Baba aliongeza kuwa pia Kanisa Halisi hufanya kazi na jamii, na kueleza sababu kuwa ni kwa kuwa Kanisa hilo ndio walipata nafasi ya kufanya kazi na jamii, tofauti na Waliotumwa (Manabii na Mitume) ambao alisema hawakupata nafasi hiyo ya kufanya kazi na jamii.

Katika uzinduzi wa Ambamu ya Bila Chanzo Halisi hutoboi sehemu ya Pili, Waimbaji waliimba nyimbo zote zilizomo katika Albamu hiyo yenye jumloa ya nyimbo 12 na kuacha umati uliofurika ukumbini ukicheza na kuwashangilia waimbaji bila kuchoka.

Aidha uzinduzi huo uliungwa mkono na wadau mbalimbali wakiwemo Benki ya CRDB ambapo baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walikuwepo wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti kwa wateja hususan waumini wa Kanisa Halisi waliokuwepo  hapo.



Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi akimpokea kwa bashasha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa alipowasili ukumbini, kushiriki uzinduzi wa Albamu ya Bila Chanzo Halisi hutoboi, katika hafla iliyofanyika jana, Aprili 28, 2024, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Hekaheka ukumbini wakati Baba Halisi na Katibu Mkuu Gerson Msigwa wakisubiriwa kuwasili.

Baba Halisi akiwasili ukumbini.
Mama Halisi akiwasili ukumbini.
Watekelezaji Sauti Wakimsubiri mgeni rasmi.
Watekelezaji Sauti Wakimsubiri mgeni rasmi.
Katibu Mkuu Gerson Msigwa akiwasili eneo la tukio.

Katibu Mkuu Msigwa akisalimia Watekeleza Sauti waliompokea.

Katibu Mkuu Msigwa akiingia ukumbini.
Katibu Mkuu Msigwa akilakiwa na Baba Halisi ukumbini.
Baba  Halisi akimwambia jambo Katibu Mkuu Msigwa baada ya kumpokea.
Baba  Halisi akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi ukumbini.
Baba Halisi akiongoza shukurani kubariki hafla hiyo.
Katibu Mkuu akishiriki kupokea shukurani hiyo.
Mama Halisi akipokea shukurani hiyo. Kulia ni Mnara Mmoja Halisi.
Baba Halisi akiwa amemuita Katibu Mkuu Msigwa kusimama mbele yake, ili apokee shukurani ya kumuinua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na viongozi wote waliopo chini ya Rais, kabla ya kuendelea zaidi na hafla hiyo.

Baba Halisi akiongoza Shukurani ya kumuinua au kumuombea Rais na Wasaidizi wake.
Mama Halisi akipokea Shukurani kutoka kwa Baba Halisi.
Washiriki wakipokea shukurani kutoka kwa Baba Halisi.
Baba Halisi akimpa maelezo katibu Mkuu Msigwa ili apokee kutiwa Damu Safi ya Chanzo Halisi (maji) kichwani ili kutimiza upokeaji shukurani ya kumuinua Rais Samia na Wasaidizi wake akiwemo yeye (Msigwa).
Baba Halisi akimmwagia kichwani damu safi ya Chanzo Halisitia Katibu Mkuu Msigwa.
Kisha Baba Halisi akainua shukurani.
Uzao na watekeleza sauti wakiwa ukumbini.
Uzao na watekeleza sauti wakiwa ukumbini.
Uzao na watekeleza sauti wakiwa ukumbini.
Uzao na watekeleza sauti wakiwa ukumbini.
Uzao na watekeleza sauti wakiwa ukumbini.
Katibu Mkuu Msigwa akizungumza baada ya kukaribishwa na Baba Halisi.
Baba Halisi na Mama Halisi wakimsikiliza kwa upendo Katibu Mkuu Msigwa.
Baba Halisi akipokea pongezi za Serikali kutoka kwa Katibu Mkuu Msigwa.
Katibu Mkuu Msigwa akikamilisha hotuba yake huku maelfu ya Uzao wakimsikiliza.
Baba Halisi na Mama Halisi wakishangilia baada ya Katibu Mkuu Msigwa kuhitimisha hotuba yake.

Baba Halisi akampongeza Katibu Mkuu Msigwa baada ya Hotuba.
Kisha wakapata picha ya kumbukumbu.

Kisha Baba Halisi akamshukuru Katibu Mkuu Msigwa.


Katibu Mkuu Msigwa akawaaga Baba Halisi na Mama Halisi kabla ya kuondoka ukumbini.




WAIMBAJI WA MOYO MMOJA WAKAINGIA  JUKWAAA UPIGA NYIMBO ZA ALBAMU YA BILA CHANZO HALISI HUTOBOI VOL II 👇👇





Watumishi wa CRDB Bank wakishiriki katika hafla hiyo. Kushoto ni Evance Mkao kutoka Makao Makuu ya benki hiyo.
Evance Makao akizungumza kueleza huduma za CRDB kwenye hafla hiyo.
Meneja wa tawi la CRDB Tegeta Martha Ngowi akijitambulisha katika hafla hiyo.
Meneja wa biashara CRDB tawi la Tegeta Stephen Makundi  akijitambulisha katika hafla hiyo.





Mtekeleza sauti Amani Halisi akitazama huduma za CRDB kwenye banda, nje ya ukumbi wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages