LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2024

SERIKALI IMEKUWA IKIIPA TBS SH. MILIONI 250, KILA MWAKA KWA AJILI YA KUHUDUMIA WAJASIRIAMALI WADOGO BILA MALIPO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dk. Athuman Ngenya, akieleza mafanikio ya Shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, katika Kikao kazi na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 15, 2024.

-----------------------------------------
 
Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Serikali imekuwa ikilipa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) zaidi ya Sh. milioni 250 kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote, ili kuweka mazingira wezeshi, ikiwemo kupata leseni za alama ya Ubora kutoka Shirika hilo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dk. Athuman Ngenya, wakati akieleza mafanikio ya Shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, katika Kikao kazi na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 15, 2024.

Dk. Ngenya amesema, kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu, jumla ya leseni 2,106 za ubora wa bidhaa  zilitolewa kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini, sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000 na kwamba, kati ya leseni hizo, jumla ya leseni 1,051 zilitolewa bure na kwa Wajasiriamali wadogo.

Alisema, pia kwa kipindi hicho wadau 5,789 kutoka mikoa mbalimbali nchini walipewa mafunzo hayo na kwamba TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo (MSEs) na wazalishaji ili kuwawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama na hatimaye kukidhi ushindani wa masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.

Kuhusu ukaguzi wa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini Dk. Ngenya alisema, Shirika limeandaa utaratibu wa kukagua viwanda vyote kuhakikisha vinazalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa, akisema kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zilitolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000.

Katika Kikao kazi hicho, Dk. Ngenya alieleza kwa kirefu utendaji wa TBS huku akiainisha mafanikio na mipango ambayo Shirika hilo linajizatiti kuitekeleza ili kuboresha huduma zake nchini. Kuyajua kwa kina yote aliyoeleza tafadhali soma taarifa kamili aliyowasilisha.

 MATUKIO ZAIDI KATIKA PICHA👇

Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akiongoza Kikao kazi baina ya TBS na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 15, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dk. Athuman Ngenya, akizungumza baada ya kukaribishwa na Kosuri, wakati wa kikao hicho.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa TBS Lazaro Msasalaga wakati wa kikao hicho.

Kosuri akiwa na baadhi ya Wahariri wa habari wakimsikiliza Dk. Ngenya.

Baadhi ya Wahariri wa habari wakiwa kwenye Kikao hicho.
Baadhi ya Wahariri wa habari wakiwa kwenye Kikao hicho.
Baadhi ya Wahariri wa habari wakiwa kwenye Kikao hicho.
Baadhi ya Wahariri wa habari wakiwa kwenye Kikao hicho.

Meneja Udhibiti Ubora wa Bidhaa ziingiazo na zinazotoka nchini wa TBS Gervas Kaisi, akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS) Dk. Ngenya, akizungumza kujibu maswali kutoka kwa Wahariri na baadaye kufunga kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages