LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 27, 2024

RC DENDEGO AMUOMBA RAIS DK. SAMIA KUPOKEA SALAM ZA WANA-SINGIDA

Hemed Munga, Iramba
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, amemuomba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupokea shukurani na salamu za upendo kutoka kwa Wanasingida, kwa kuendelea kuujali mkoa huo kwa kuupa wataalamu na fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo katika nyanja zote.

RC Dendego ametoa ombi hilo, wakati akifikisha salam za Rais  Dk. Samia kwa wananchi wa mkoa huo, katika Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano zilizofanyika katika Kiwanja cha Stendi mjini Kiomboi, wilayani Iramba, jana.

"Tunasema asante sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wewe na serikali unayoiongoza, " akasema RC Dendego.

Amesema, miongoni mwa mambo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dk. Samia imeyasimamia Aidha, ameeleza kuwa yapo mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo, hivyo mkoa huo hauna njaa.

Pia, ameongeza kuwa wamepiga hatua kubwa kwa sababu wanapata maji safi na salama, hospitali, vituo vya afya, zahanati, shule na barabara za lami.

Kutokana na hayo,  Dendego amewataka  wananchi hao kuendelea kudumisha utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kwa lengo la kuhakikisha siku zote wanakuwa salama.

"Ndugu zangu,  mimi ni muumini wa kazi, mafanikio na furaha, hivyo ninataka watu wote ninaowaongoza wawe wanacheka na kufurahi tunapokutana, sitaki kuona machozi," amesisitiza.

Hata hivyo, RC Dendego amempongeza Mkuu wa wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda kufuatia hali iliyojitokeza ya kutokupatikana mwananchi mwenye kero baada ya kiongozi huyo kutoa nafasi tatu kwa wanawake na nyinge tatu kwa wanaume.

"Mheshimiwa DC hongera sana, hii sio kawaida inaelekea unachapa kazi kweli kweli, endelea hivyo hivyo mdogo wangu, kazia hapo hapo hakuna kurudi nyuma," amempongeza.

Amesema kuwa kwa sababu  hakuna kero, waendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuwafanya Watanzania kuwa wamoja, Taifa moja lenye historia ya damu na udugu wa asili.

Kwa upande wa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa huo, Elphas  Lwanji  amewasilisha salam za  Mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Martha Mlata kuwa chama hicho kinaimani na RC Dendego kuwa atawaongoza vizuri katika mkoa huo.

Aidha, amewataka wanachi hao kutembea kifua mbele kwa sababu serikali yao imeendelea kufanya mambo makubwa  kwa ajili yao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amesema katika kuadhimisha miaka 60 ya  Muungano walizindua na kuweka kambi ya siku takribani tano ya Madaktari Bingwa na Bobezi  katika hospitali ya wilaya hiyo.

Aidha, amesema kuwa katika kipindi cha muda huo mchache Madaktari hao Bingwa wameweza kuwaona na kuwahudumia wagonjwa 587.

Pia, amesema wamefanya upasuaji wa macho, mifupa na upasuaji wa jumla kwa wagonjwa takribani 80.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, kwa kweli kambi yetu imekua ya mafanikio makubwa sana, tulipokea wagonjwa kutoka Iramba na wilaya ya jirani Igunga mkoani Tabora," amesema DC Mwenda.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Halima Dendego akizungumza na wananchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika kimkoa katika kiwanja cha stendi mjini Kiomboi wilayani Iramba.

Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Mwenda akizungumza, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika kimkoa katika kiwanja cha stendi mjini Kiomboi wilayani humo.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapindunzi (CCM) mkoa wa Singida, Elphas Lwanji akizungumza, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika kimkoa katika kiwanja cha stendi mjini Kiomboi wilayani Iramba mkoani hapa. (Picha zote na Hemedi Munga)

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages