LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2024

RAIS SAMIA ATUNUKU NISHATI VIONGOZI WASTAAFU MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, IKULU, CHAMWINO, DODOMA, LEO

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli, Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtunuku Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tluway Sumaye kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.(Picha na Ikulu).

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages