LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 29, 2024

RAIS DK SAMIA AONGEZEA TENGEO LA BAJETI YA UTAFITI KWA TUME YA NGUVU ZA ATOMU HADI KUFIKIA SH. MILIONI 450

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeongeza tengeo
la bajeti ya utafiti kwa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) hadi kufikia Sh. milioni 450 katika
mwaka wa fedha 2023/2024.

Juhudi hizo za serikali zimefanyika ili kupata fursa zaidi za sayansi na teknolojia ya nyukilia na pia kuwalinda wananchi na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi na kwamba katika miaka mitatu machapisho 25 yakitafiti yameshapatikana katika juhudi hizo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAEC) Prof. Lazaro Busagala akieleza baadhi ya mafanikio ya utendaji wa Tume hiyo, katika kipindi cha Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia, katika kikao kazi chake na Wahariri na Waandishi wa Habari, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Aprili 29, 2024.

Katika kikaokazi hicho ambacho kiliandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo la TAEC kuujulisha umma juu ya maendeleo ya utendaji wake, Prof. Busagala amesema, katika kipindi hicho Tume hiyo imepaa kimafanikio, akampongeza na Kumshukuru Rais Dk. Samia kutokana na mafanikio hayo.

Amesema, kutokana na TAEC kuwa imara kiutendaji, makusanyo yake ya maduhuli ya serikali yamepanda kutoka Sh. bilioni 8.7 mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia Sh. Bilioni 10.9 mwaka wa fedha 2022/2023, Prof. Busala akisema, mafanikio hayo yametokana na juhudi za Serikali ya awamu ya Sita kufungua ofisi za kanda, mipakani na kutumia mifumo ya TEHAMA kama vTANCIS, TeSWS na EDMS katika kutoa
huduma.

Prof. Busagala ameeleza mafanikio lukuki japo kwa mujibu wa maelelezo yake mafanikio aliyoeleza siyo yote, lakini kwa namna alivyoyawasilisha katika kikao kazi hicho 'yameshiba'. Tafadhali soma taarifa kamili kama alivyoiwasilisha.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC) Prof. Lazaro Busagala akieleza baadhi ya mafanikio ya utendaji wa Tume hiyo, katika kipindi cha Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia, katika kikao kazi chake na Wahariri na Waandishi wa Habari, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Aprili 29, 2024.

TAARIFA KAMILI KAMA ALIVYOIWASILISHA PROF. BUSAGALA 👇

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages