Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella, ametuma salam kwa waliokuwa hawamuelewi Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwa watambue kwamba kwa safu mpya ya Sektarieti ya CCM sasa ndiyo 'muziki' umeanza.
Mongella ametuma salamu hizo, wakati akihutubia katika mkutano wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekretarieti wapya wa CCM, yaliyotimua vumbi, leo kwenye Viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na mamia ya wana CCM na wananchi kwa jumla.
“Mimi kwa nafasi yangu kama Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara sio mtu wa majukwaa sana, ninawaahidi nitasimamia kuhakikisha utendaji ndani ya Chama chetu unaakisi ukubwa wa Chama. Kama Mtu ana akili timamu baada ya kumsikia hapa Jokate, Ally Hapi na Makalla, maana yake muziki umeanza na Mimi nataka kusema kama kuna Mtu alikuwa hamuelewi vizuri Mh. Rais Dkt. Samia hii safu ni ujumbe tosha.
Kazi yetu ni kujipanga na Wana CCM tuwe na kujiamini. Kuna maeneo Wana CCM wanatishwa kitotototo, tusikubali kutishwa na yeyote, Mimi nakumbuka (akiwa UVCCM) tulipiga marufuku watu kutishwa hapa mjini, ilikuwa marufuku Watu kutishwa Mtu akitaka aje kistaarabu, Vijana lazima tusimame kukilinda Chama”. Akasema Mongella na kuongeza;
"Na mmepata Mwenyekiti imara, Katibu Mkuu Imara, Viongozi wote imara, UVCCM mna jukumu la kulinda Viongozi wa Chama na mali za Chama, wote tuna Dini zetu na Madhehebu yetu lakini CCM sio Dini wala dhehebu ina kazi ya kutafuta Dola, kwahiyo katika kushika Dola hakuna kubembelezana.
Katika kutafuta Dola hakuna Shangazi wala Mjomba, tukimaliza kushika Dola Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu tutakuja tutakaa mezani tutakunywa kahawa, na jambo hili wala halina mzaha lakini kama wenzangu walivyosema Mh. Rais ni Muumini wa maridhiano na mapatano na demokrasia ya kweli”.
“Tungeomba wote uwe mwelekeo wetu mpaka Vyama rafiki, lakini pale Mtu akikata kwenda vinginevyo sisi huku hasa kwenye Sekretarieti hii utaalamu upo wa kutosha wa hayo mengine lakini tutakuwa wavumilivu kwasababu Mwenyekiti wa Chama chetu anaamini katika hilo lakini ushindi wa CCM ni lazima wala halina mjadala”.
Wajumbe wapya wa Sekretarieti yaliopokewa katika mapokezi hayo wakiongozwa na Mongella ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ally Hapi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo.
Kunogesha mapokezi hayo, Wajumbe hao walifuatana na Mjumbe mwenzao wa Sekretarieti, Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Haji Ussi Gavu.
Wengine katika utimilifu wa sekretarieti ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Dk. Frank Awasi, Katibu wa NEC, SUKI Rabia Abdallah Hamis, ambao siyo katika kundi lililoteuliwa jana. Nafasi ya Mjumbe wa Sekretarieti iliyobaki wazi ni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) aliyoondolewa Jokate kwenda UVCCM.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara John Mongella akipongezwa na Mwrnyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtevu baada ya hotuba yake kwenye mapokezi hayo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Amos Makalla akihutubia na kumkaribisha Mongella kuhutubia katika mapokezi hayo.
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Haji Ussi Gavu akihutubia katija mapokezi hayo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ally Hapi akihutubia katika mapokezi hayo.
Katibu Mkuu wa UVCCM Jokate Mwengelo akihutubia katika mapokezi hayo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Amos Makalla akifurahia jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Adam Ngalawa.
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Wajumbe wapya wa Sekretarieti wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtevu, Issa Haji Ussi Gavu na Adamu Ngalawa (kulia), waliopokuwa wakiwasili kwenye mapokezi hayo.
Shamrashamra zikitanda wakati wa mapokezi hayo.
Shamrashamra zikitanda wakati wa mapokezi hayo.
Shamrashamra zikitanda wakati wa mapokezi hayo.
Shamrashamra zikitanda wakati wa mapokezi hayo.
Cde Mongella.
Cde Makalla
Cde Hapi
Cde Jokate.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇