Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ameeleza kuwa CCM itaendelea kutatua kero za wananchi lakini bila kuingilia kesi zilizopo mahakamani kwani kufanya hivyo ni kuingilia majukumu ya mhimili wa mahakama jambo ambalo halitakiwi.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dkt. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati kuwasalimia makada wa chama waliofika kuwalaki Ofisi za CCM Mkoa wa Katavi mjini Mpanda.
Dkt. Nchimbi ambaye katika ziara hiyo ameambatana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇