LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2024

DKT NCHIMBI: TOENI VIBALI KWA WAKULIMA KWELA KUUZA MAHINDI NJE YA NCHI

 



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi  akihutubia wananchi waliomsimamisha wakiongozwa na Mbunge la Kwela, Deus Sangu katika Kijiji cha Chombe, mkoani Rukwa  wakimuomba azipatie ufumbuzi kero zao za ukarabati wa shule, Kituo cha Afya n, miundombinu ya barabara na wakulima kupewa kibali cha kuuza mahindi yao nchi ya za jirani.

Nchimbi ambaye msafara wake ulikuwa unatokea Sumbawanga Mjini kwenda Songwe,baada ya kusikiliza kilio chao hicho, aliwaagiza mawaziri wanaohusika na kero hizo kufanya jitihada za kuzipatia ufumbuzi ikiwemo Wizara ya Kilimo kutoa vibali vya kuuza mahindi katika nchi jirani na kuwaahidi kuwa mahindi hayo yatanunuliwa na serikali. Aliwasihi wakipewa vibali wasiuze mahindi yote wabakize kwa ajili ya chakula.


Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea kesho katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.

Mbunge wa Kwela, Deus Sangu akiwasilisha kero hizo kwa niaba ya wananchi.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na  Mafunzo, Amos Makalla akisema neno la utangulizi kuhusu kero hizo kabla ya kumkaribisha Dkt Nchimbi kuzungumza na wananchi hao pamoja na kuwaagiza viongozi wahusika pamoja na mawaziri kuzitafutia ufumbuzi wa haraka baadhi ya kero hizo.
Wananchi wakionesha furaha yao baada ya Dkt Nchimbi kuwahakikishia kuwa baadhi ya  kero zao zitatafutiwa ufumbuzi.





IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages