LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 20, 2024

DKT NCHIMBI ALAKIWA KICHIFU NYUMBANI SONGEA RUVUMA


 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Emmanuel Nchimbi akikaribishwa rasmi nyumbani kwao Mkoa wa Ruvuma kwa kufanyiwa kimila na machifu pamoja na wazee wa  jadi alipofika eneo la Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Maji Maji mjini Songea Aprili 20, 2024.


Katika ziara hiyo, Dkt. Nchimbi  ameambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

 Kiongozi huyo mtendaji mkuu wa CCM, atakuwa mkoani Ruvuma ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku 10 katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya na Njombe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma.



Akikabidhiwa silaha za jadi



Akiwa eneo la Mnara ambapo alifanyiwa tambiko.


Dkt Nchimbi akizungumza na wazee wa kimila mbele ya Mnara wa  walipozikwa mashujaa 67 wa vita vya maji maji  walionyongwa na utawala wa kijerumani.




Dkt Nchimbi na viongozi wengine wakiwa eneo la kaburi la Chifu Songea Mbano aliyeongoza vita hivyo vya maji maji. Alinyongwa mara tatu bila mafanikio na hatimaye kupigwa risasi. Hapo kilizikwa kiwiliwili baada ya kukatwa kichwa  na wajerumani na kuondoka nacho. Serikali imedai kichwa hicho kirejeshwe nchini lakini hadi sasa hakijarejeshwa.






 Akiondoka baada ya kutembelea eneo hilo la Mnara wa mashujaa na Kaburi la Chifu Songea.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
0754264203

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages