LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2024

DK. NCHIMBI: TUTAENDELEA KUWACHUJA VIONGOZI WETU BILA HAYA, WASIO NA MOYO WA UTUMISHI HAWATAPATA NAFASI YA KUTUMIKIA CHAMA

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema kutokana na dhamiara ya tangu kuasisiwa kwa vyama vya TANU na ASP, ni busara kila Mtanzania kuungana na Chama Chama Mapinduzi katika kuendelea kupambana na kero, kwa kuwa ndiyo chama pekee kinachoweza kujinasibisha na kero za wananchi na maisha ya kawaida ya mwananchi.

Balozi Dk. Nchimbi ameyasema hayo, leo mjini Nkasi wakati akizungumza na wananchi akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Rukwa, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.

"Nachoomba kwenu mjue kwamba Chama Cha Mapinduzi, tangu kuasisiwa kwake kimejizatiti kuwa chama cha watu, kutumikia watu, hiki ni chama ambacho msingi wake unaanzia na vyama vya TANU na ASP ambavyo vilikomboa nchi yetu lakini vyoye vilijikita katika matatizo ya kawaida ya wananchi, vyote viljikita katika kumkomboa Mtanzania na Umasikini, ndiyo maana kauli mbiu ya kwanza kabisa ya vyama vyetu vya awali ilikuwa maadui zetu wakuu ni magonjwa, umasikini na maradhi.

Ndiyo maana kazi kubwa iliyofanywa kwa miaka yote tangu tulipopata uhuru ni kupambana na maadui hawa, kujenga shule za kutosha , hospitali, miundombinu ya kilimo na barabara kuona kwamba tunamkomboa Mtanzania kutokana na umasikini", akasema Balozi Dk. Nchimbi.

Balozi Dk. Nchimbi akasema, kutokana na sababu hizo kiongozi wa CCM anapimwa kwa uwezo wake wa kutumikia watu, hapimwi kwa uwezo wa kujinufaisha binafsi, kunufaisha familia yake, anapimwa kwa uwezo wa kutumikia watu.

"Na kadri huku tunapokwenda tunaendelea kuchuja viongozi wetu na tutakuwa tunawachuja bila haya, wale ambao hawana moyo wa utumishi hawatapata nafasi ya kutumikia katika chama chetu.

Kwa hiyo tunawaomba wananchi muendelee kukiunga mkono chama chenu (CCM) mjue hiki ndiyo chama pekee ambacho kina dhamira ya dhati, kina viongozi wanaoweza kutekeleza dhamia hiyo lakini pia kina utayari wa kutekeleza dhamira hiyo ya kupambana na umasikini wa watu wetu.

Sisis kama Chama Cha Mapinduzi, tukachokitekeleza kwa nguvu zetu zote ni kuhakikisha kwamba serikali zetu wakati wote zinajielekeza katika kutumikia wananchi, hatutasita kukosoa, hatutasita kuelekeza  lakini wote tukijikita katika kufanikisha maendeleo ya nchi yetu", akasema Balozi Dk. Nchimbi na kuwaambia wananchi wa Rukwa;

"Na kwa bahati nzuri mna kada mzuri, kamisaa wa Chama katika mkoa wetu, Makongoro Nyerere, huyu kila nikiomuona namkumbuka Baba wa Taifa, kwa sababu wote mnajua utumishi wake alioutoa kwa nchi yetu, mimi binafsi huwa sioni haya kusema mimi ni mfuasi asiyeyumba wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa jinsi alivyoipenda nchi yetu alivyotumia akili na maarifa yake kuhakikisha nchi yetu inaendelea bila yeye kujinufaisha.

Mnakumbua juzi  tulipata hela za Uviko 19, baadhi ya nchi nyingi za Kiafrika walitumia kugawana hela viongozi, walinunulia magari ya kifahari, lakini sisi Tanzania Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,  akasema sisi tutapekela kujenga hospitali, shule, dawa, hele zote zikatawanywa mikoani na wilayani hakuna hata moja iliyobaki Ikulu.

Sasa mwanzoni nilidhani ni mimi ndiye mfuasi wa Nyeyeye, kumbe Mama Samia naye ni mfuasi. angekuwa mtu mroho hela angekusanya tu zile hela halafu angegawana na rafiki zake na familia yake. hela zimekwisha. Na mtu akishakuwa rais asikudanganye mtu akiamua kuwa mbabe inakuwa shida sana.

Lakini sisi tuna rais mzalendo, mwanademokrasia, anaruhusu watu kusema, kuongea, ukishapa uhuru wa kusema unakuwa pia na uhuru wa kuwaza, kwa hiyo tukishakuwa na uhuru tuutumie vizuri, tusikebehiane tusidhauliane", akasema Balozi Dk. Nchimbi.

Baada ya hotuma yake, Balozi Dk. Nchimbi alimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla ambaye wakati akihutubia alikuwa (Makalla) akisikiliza kero za wananchi mbalimbali.

"Kwa muda huu niliokaa faragha nimewasikiliza wananchi 16, tukiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa wilaya anayekaimu. hapa Nkasi katika kero zote, mbili tu ndizo zenye ngazi ya kitaifa lakini nginie zinaishia hapa katika wilaya hii katika mkoa huu, kwa sababu wanaojibu kero hizi wapo. wanatakiwa wazijibu ziishe tukija tena au akija kiongozi mwingine, tusikie kero mpya.

Mapema, Balozi Dk. Nchimbi akizungumzia kero ya Maji na kuwasiliana moja kwa moja kwa simu na Waziri Maji Juma Awesso ambaye aliwahi kuahidi kupeleka  Sh. milioni 700 kwajili ya mradi wa maji, zikapelekwa Sh. milioni 300, hivyo Balozi Dk. Nchimbi akamtaka Waziri huyo awaambie wananchi zitapekekwa lini Sh. milioni 400 zilizobaki kukamilisha mradi.

"Mkuu hayo ni maelekezo, Rais Samia alishaelekeza hataki kuona kina mama wanahangaika na maji. nataka nikuhakikishie mheshimiwa Katibu Mkuu, kesho Jumatatu, namueekeza Katibu Mkuu wa wizara ya maji hizo milioni 400 zote zitoke zikakamilishe mradi wamaji

Kwa sababu maelekezo ya chama kwetu sisi ni utekelezaji tu. Nataka nikuhakikishie wizara ya maji hatutakuwa kikwazo katika kuhakikisha dhamira ya rais kumtua mwamama ndoo kichwani na ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa" akasema Waziri Awesso.

Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages