LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 22, 2024

DK NCHIMBI AIFARIJI FAMILIA YA MWASISI WA TANU MBINGA

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt, Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mwasisi wa  Chama cha TANU, marehemu Costantine Millinga mjini Mbunga, mkoani Ruvuma Aprili 22, 2024.

Dkt Nchimbi amesisitiza kuwa chama kitaendelea kiwaenzi waasisi wote wa chama hicho kwa kazi kubwa waliolifanyia Taifa hili.

Katika tukio hilo aliambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu. 

Dkt Nchimbi akimsalimia na kumpa pole, Mary mjane wa marehemu Millinga.
Akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla akiweka shada la maua kwenye kaburi la mwasisi hiyo ambaye pia alikuwa mmoja wa viongozi wa Chama cha TAA (Tanganyika African Association) kilichozaa TANU.
Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu akiweka shada la maua.
Kiongozi wa Dini akiongoza ibada maalumu ya kumbukumbu ya kifo cha Mzee Millinga.
Mjukuu wa marehemu, BeatriceMillinga akisoma wasifu wa marehemu Millinga.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amezuru kaburi la Hayati Mzee Constantine Osward Millinga, aliyekuwa mmoja wa waasisi na wapigania uhuru kuanzia wakati wa Tanganyika African Association (TAA), Tanganyika African National Union (TANU), hadi CCM, katika makaburi ya familia yaliyopo, Mtaa wa Mhekela, Mbinga Mjini, mkoani Ruvuma, leo Jumatatu, Aprili 22, 2024.


Katibu Mkuu wa CCM Dk Nchimbi, na viongozi aliombatana nao katika msafara wa ziara yake mkoani humo, mbali ya kuweka shada ya maua, walipata nafasi ya kumsalimia Mjane wa Hayati Millinga, Bi. Maria Orign Mapunda (88), na kushiriki ibada ya kumuombea marehemu iliyoongozwa na Padri Andrea Silimbo. 


Hayati Mzee Millinga ambaye alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa TAA, TANU hadi CCM, akishirikiana na wenzake, wakiwemo viongozi wakuu na wanachama, wakiongozwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa sehemu ya waasisi wa vyama hivyo vya ukombozi vilivyobeba chimbuko na kuweka misingi ya uhuru na maendeleo ya Tanganyika, baadaye kuipata Tanzania, na kuzaliwa kwa CCM, alifariki dunia Machi 5, 2018. 


Akizungumza wakati wa kutoa salaam za pole kwa wanafamilia na wananchi wengine,  Dk Nchimbi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuenzi na kujifunza kupitia mema yote yaliyofanywa na waasisi wake wa vyama vya TANU na ASP, ikiwa ni sehemu ya njia ya kuendelea kulijenga Taifa letu kwa misingi imara ya kisiasa, uchumi na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa. 


Dk Nchimbi aliambatana na Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndugu Issa Haju Gavu na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makala.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages