Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akijadiliana jambo na Balozi wa Shina namba 5, Mtaa wa Paradise, Majengo mjini Mpanda, Hadija Ally Kapena alipokwenda kuhushuria kikao cha shina hilo kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama, kutatua kero na utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Dkt. Nchimbi amefurahishwa na taarifa ya shina hilo kwamba hali ya usalama katika eneo hilo iko shwari, uhai wa chama uko vuzuri. Aidha alitoa maelekezo kwa viongozi wote wa chama kuanza kutatua kero za wananchi kuanzia ngazi ya matawi, mashina, kata, wilaya akidai huko ndiko kwenye chimbuko la chama.
Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama,kuhudhuria vikao vya baadhi ya mabalozi wa mashina, kusalimia wananchi na kutatua kero, kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Makalla akisaini kwenye kitabu cha kumbukumbu cha shina hilo.
Dkt. Nchimbi akisalimiana na baadhi ya makada wa CCM
Baadhi ya wabunge wa majimbo na viti maalumu wa mkoa huo wakiwa katika shina hilo.
Balozi na Mwenyekiti wa Shina, Hadija Kapena akiongoza kikao na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Nchimbi kuzungumza katika kikao hicho.
Makalla akitoa neo wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wanachama na wajumbe wa kikao hicho waliohudhuria kikao hicho.
Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu akielezea umuhimu wa vikao vya shina na viongozi wazuri wanaotakiwa kukiongoza chama hicho.
Balozi wa shina namba 5 Mpanda Mjini, Hadija Kapena akiwa na furaha kuhusu ujio wa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Nchimbi katika Shina hilo.
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇