LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2024

DK. NCHIMBI AAGIZA UJENZI UWANJA WA SUMBAWANGA UJENGWE KWA UBORA UNAOTAKIWA


 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwaongoza viongozi wa chama na serikali kukagua maendeleo ya ujenzi Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga wakati wa ziara yake mkoani Rukwa Aprili 15, 2024.

Dkt Nchimbi ameagiza wakandarasi kukamilisha ujenzi Machi mwakani na kwa ubora unaotakiwa. Ujenzi wa  uwanja huo utakaogharimu zaidi ya sh. Bil. 60 utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 150, 000 kwa mwaka na utarahisisha zaidi usafiri kwa wakazi na wageni.  Watu 120 wamepata ajira katika mradi huo ambapo wazawa wamekuwa 114.


Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea kesho katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.




Dkt Nchimbi akiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Rukwa, Sultan Seif wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa uwanja huo.
Dkt Nchimbi akikagua ujenzi wa jengo la abiria uwanjani hapo.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mgeni Mwanga.
Dkt Nchimbi akinong'onezwa jambo na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla.
Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja huo, Licoi Laban wa Kampuni ya SMEC akitoa maelezo kwa Dkt Nchimbi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo.
Dkt Nchimbi akitoa maagizo baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo.
Dkt. Nchimbi akiondoka baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages