LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 19, 2024

DK MHAGAMA AKABIDHI KWA CCM MALI ZAKE ZA SH. MIL 45, DK NCHIMBI AMPONGEZA

Mbunge wa Madaba, Joseph Mhagama akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi hati na nyaraka zingine za viwanja vyake viwili na mabanda ya biashara vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 45 kuwa mali ya CCM.


Makabidhiano hayo yamefanyika eneo la viwanja hivyo wakati Dkt Nchimbi aliposimama kuwasalimia wananchi katika Jimnbo la Madaba akitokea Njombe tayari kuanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma Aprili 19, 2024.


Nchimbi amempongeza Mbunge huyo kuwa kuwa na moyo wa kutoa mali kwa ajiliya chama na kwamba wanachama wa namna hiyo ndiyo wanaotakiwa kwenye chama hicho.

Dkt Nchimbi akikabidhi baiskeli kwa baadhi ya viongozi wa mashina zilizotolewa msaada na Mbunge wa Madaba, Dkt Joseph Mhagama.


Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Dkt Nchimbi kuzungumza na wananchi.
Baadhi ya makada wa CCM wakishudia makabidhiano hayo.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
0754264203
 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages