LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 17, 2024

AMSHA AMSHA YA MAPOKEZI YA DKT NCHIMBI MBEYA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akilakiwa kwa mashamushamu alipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya katika kikao chaa ndani cha Kamati ya Siasa Aprili 17, 2024.

Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea leo katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.
Dkt Nchimbi  akipokea zawadi ya shada la maua kutoka kwa Kamanda wa Chipukizi Mkoa wa Mbeya, Razia Yusufu.

Akisalimiana na baadhi ya makada wa CCM.

Dkt Nchimbi akiupongeza Mkoa wa Mbeya kwa mapokezi mazuri.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla akijitambulisha.


Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu akijitambulisha.

Shamrashamra za mapokezi.




IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203
 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages