Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GTB) imesema, mchango wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha imechangia katika mapato ya serikali kwa ongeko la kodi kutoka Sh. bilioni 33.6 Mwaka 2016/17 hadi kufikia sh. bilioni 170.4 mwaka 2022/23, ikiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 407.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, katika Kikao Kazi na Wahariri na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo (GTB) James Mbalwe amesema sekta hiyo ya michezo ya kubahatisha katika mapato hayo ni sehemu ya sh. bilioni 108.16 zilizokusnywa katika kipindi cha 2023/2024.
Amesema pia GTB imefanikiwa kuokoa mapato ya Serikali ya Sh. Bilioni 2.44 ambayo serikali ingeyakosa, kama Bodi hiyo isingefanikiwa kukamata mashine 1,846 za waendeshaji haramu wa michezo ya kubahatisha katika maeneo mbalimbali nchini, katika kipindi cha kati ya mwaka 2018 na 2022.
Mbalwe, amesema, kwa upande mwingine GTB imefanikiwa kuchangia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa mujibu wa kuanzishwa kwake na haijawahi kupata hati chafu ya ukaguzi tangu kuanzishwa kwake na kwamba utendaji bora wa Bodi hiyo imeifanya Tanznaia kuwa mfano kwa baadhi ya nchi za Afrika, kati na Kusini ukiondoa Afrika Kusini.
Amesema kutokana na mafanikio TGB imekuwa mwalimu kwa baadhi ya nchi zikiwemo Kenya, Uganda, Zimbabwe, Malawi na Ethiopia. katika kipindi cha kati ya mwaka 2018. 2019 hadi Agosti 2022.
Taarifa yote ya TGB iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu Mbalwe, hii hapa👇
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GTB) James Mbalwe akizungumza katika kikaokazi na Wanahrir na Waandishi wa Habari, leo jijini Dar es Salaam.




















No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇