LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 27, 2024

RC MAKALLA AUFAGILIA UONGOZI WA CHATANDA KWA KUWAJALI WANAWAKE

 














Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makala ameupongeza uongozi wa Mary Pius Chatanda Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania jinsi ambavyo umejidhatiti kuwajengea uwezo Viongozi Wanawake kutoka makundi mbalimbali. Hayo yamebainika baada ya Mhe Chatanda kutembelea Ofisi za mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwa na ziara ya Siku moja Mkoani humo. Mhe Makala amesema, anaiona UWT madhubuti iliyojidhatiti na mikakati endelevu katika kuwakwamua wanawake. Hivyo anafarijika kuona UWT imewezesha mafunzo kwa viongozi wanawake. 


Kadharika, Mhe Chatanda akiwa ofisini humo amesema, yupo Mkoani Mwanza kwaaajili ya mafunzo maaalum ya uongozi kwa viongozi wanawake wa Mikoa 9 ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi ili kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi na kijamii.


Mhe Chatanda ameambatana na Katibu Mkuu UWT Ndg. Jokate Mwegelo, Naibu katibu Mkuu UWT Bara Ndg. Riziki Kingwande, na viongozi mbalimbali kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kigoma na Mara pamoja na Mhe. Amina Makilagi Mkuu wa Wilaya Nyamagana . 



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages