MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, ndugu Mwajuma NYAMKA (pichani) amewashukuru viongozi na wana CCM kwa ujumla kwa kufanikisha ushindi wa kishindo wa udiwani katika uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata ya Msangani.
"Ninawashukuru Wanaccm wa Wilaya Kibaha Mjini hususani wa Kata ya Msangani na Wananchi wa Msangani kwa Kukiamini Chama Cha Mapinduzi na Kukiheshimisha kwa Kukipatia kura za kishindo kwenye uchaguzi mdogo wa Udiwani uliomalizika tarehe 20 March 2024 na Kumpata ndugu Gunze Yohana Chongela" anasema Nyamka.
Anaongeza kuwa "Sina Maneno mazuri yenye thamani na imani yao walioionyesha kwa Chama cha Mapinduzi zaidi ya kusema AHSANTENI SANA na kuwahidi Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuwa kimbilio la Wananchi na kitahakikisha kinasimamia Maendeleo yanafika".
Katika uchaguzi huo mgommbea wa CCM, Yohana Gunze wa Kata ya Msangani Wilaya ya Kibaha Mjini amepata Kura 5862 Kati ya kura halali 5909 sawa na asilimia 99.20. Katika Kata ya Msangani palikuwa pia na wagombea wengine kutoka vyama vya ADA - TADEA, CCK, DEMOKRASIA MAKINI, DP, N.R.A, UMD na UPDP.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇