LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 19, 2024

KISHINDO CHA UTENDAJI WA RAIS DK, SAMIA KATIKA MIAKA MITATU MOTO, TFS YAINGIZA BILIONI 371.9 NA KUWASILISHA BILIONI 62.9 KATIKA MFUKO WA SERIKALI

Kamishna wa Uhifadhi wa TFS Prof. Dos Santos Silayo, akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Machi 19, 2014.

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Kishindo cha ufanisi wa utendaji wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake tangu alipoapishwa Machi 19, 2021, kimezidi kutikisa kila sekta, ambapo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) nao umejitokeza na kueleza bayana kwamba katika kipindi hicho umepata mafanikio lukuki yaliyokuwa hayapata kutokea.

Akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Machi 19, 2014, Kamishna wa Uhifadhi wa TFS Prof. Dos Santos Silayo amesema kutokana na kupata mafanikio katika utendaji wake ndani ya kipindi cha miaka hiyo mitatu, Wakala umekusanya jumla ya sh. Bilioni 371.9 (Sh. 371,956,374,658.38).

Kamishna Prof. Silayo amesema kufuatia makusanyo hayo TFS ndani ya miaka hiyo mitatu imeweza kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali Sh. Bilioni 62.9 (Sh. 62,900,000,000) ikiwa ni sawa na asilimia 15 ya makusanyo.

Amesema, katika mazao ya misitu nje ya nchi, uuzaji bidhaa za misitu nje ya nchi uliongezeka kwa asilimia 87 kutoka meta za ujazo 227,615 mwaka 2020/21 hadi meta za ujazo 426,805 kwa mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa kwa upande wa mbao zolizohandisiwa. mauzo nje yaliongezeka toka meta za ujazo 15,876
hadi 47,491 (asilimia 66.6).

Kamishna Prof. Silayo amemshukuru Rais Dk. Samia, akisema juhudi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita zimewezesha kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea vituo vya utalii ikolojia kutoka 59,606 mwaka 2020/2021 hadi kufikia 242,824 mwaka 2022/2023 na mapato katika kipindi hicho kuongezeka kutoka Sh.154,965,050 hadi kufikia wastani wa Sh. 1,5018,940,965.

"Haya ni mafanikio makubwa kupatikana na Wakala katika sekta ya utalii eneo la utalii ikolojia kuliko wakati mwingine wowote", alisema  Kamishna Prof Silayo.

Kamishna Prof. Silayo amesema kufuatia mafanikio hayo,  Wakala ulifanikiwa kugawa miche yenye thamani ya Sh. Bilioni 12.47, mizinga 2,256 yenye thamani ya Sh. 244,500,000, Msaada wa ujenzi wa miundombinu
ya thamani ya Sh. Bilioni 1.63 kwa jamii zinazozunguka misitu.

Kwa uchache hayo ni miongoni mwa mafanikio aliyoyataja Kamishna Prof. Silayo katika Kikao Kazi hicho. Kuyajua yote, Tafadhali soma taarifa taarifa kamili kama alivyoiwasilisha.👇

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages