Na Official CCM Blog, Dar es Salaam.
Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Marekani (USA), Salma Moshi, kwa niaba ya wanachama na wapenzi wote wa CCM tawi hilo, ametuma salamu za pole kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi, Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki na Watanzania wote, kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Pili Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi kilichotokea tarehe 29 Februari, 2024 saa 11.30 Jioni katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.
"Hakika mimi na Wanachama wenzangu wa CCM tawi la USA, tumepokea taarifa za msiba huu wa kitaifa kwa majonzi makubwa. Tunawapa pole Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi, Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki na Watanzania wote kufuatia kifo hiki. Tunawaomba wote Mungu awajaalie subira katika kipindi hiki kigumu cha majozi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
TUNAMUOMBA ALLAH AMPE QAUL THABITI MZEE WETU ALHAJ ALI HASSAN MWINYI.
Inna Lillah waina Ilayhi Rajiuun", amesema Salma Moshi katika salam hizo za pole.
Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Marekani (USA), Salma Moshi alipokuwa na Mzee Mwinyi na Mama Mwinyi. Mzee Mwinyi alikuwa kipenzi cha watu.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇