KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Khadija Ali Salum (pichani) amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa utendaji bora.
Mwanasiasa huyo maarufu anasema katika miaka mitatu ya mafanikio ya Dkt. Samia hakika amefanya makubwa yanayopaswa kusifiwa na kila mpenda maendeleo.
Akaongeza kuwa “ningependa kuhamasisha kina mama na vijana kwa ujumla kumuunga mkono mwanamke huyu shupavu ambaye alipata nafasi ya kuiongoza Tanzania katika kipindi kigumu ambacho Watanzania hatukutarajia kabisa kama tungepatwa na msiba wa kiongozi ambaye yuko madarakani.
Lakini kwa neema za Mungu leo hii mama ametuongoza vyema ndani ya miaka hii mitatu katika sekta mbalimbali na kufanikisha maendeleo lukuki kwa mfano sekta ya Kilimo Serikali imefanikiwa kuongeza bajeti ya kwa asilimia 29 (2022-2023) kutoka Bilioni 751 hadi Bilioni 970.
Pia elimu, Serikali imefanikiwa kunufaisha wanafunzi 14,920,103. Serikali imetumia Bilioni 660.7 kwa mfano katika ujenzi wa madarasa 10,678, nyumba za walimu 353 na maabara 1,356
Elimu ya juu imetoa mikopo yenye thamani ya sh. Trilion 1.669 kwa wanafunzi 380,654.
Barabara, kwa upande huu Serikali imefanikiwa kujenga kilomita 15,625.55 ambapo utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali.
Your Ad Spot
Mar 22, 2024
Home
Unlabelled
KATIBU WA SUKI KHADIJA ALI SALUM AMPONGEZA RAIS SAMIA
KATIBU WA SUKI KHADIJA ALI SALUM AMPONGEZA RAIS SAMIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇