LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 24, 2024

KAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA JENGO LA PSSSF COMMERCIAL COMPLEX

Na K-VIS Blog/Khalfan Said
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), imesema imeridhishwa na uwekezaji wa Jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex, lililoko barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo la kisasa lenye ghorofa 35 linamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kwa sasa tayari limekamilika kwa asilimia 100 na limeanza kutumika.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya PIC ya kutembelea mradi huo wenye thamani ya sh. bilioni 232, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge Mhe. Deus Sangu amesema, Kamati imekagua mradi na kujiridhisha kuwa ni mzuri na umetekelezwa kwa viwango vyote vinavyohitajika.

“Sisi kama kamati tumeendelea kuishauri PSSSF kuhakikisha jengo hili ambalo limewekeza fedha nyingi za Mfuko linasimamiwa na tija iliyokusudiwa inapatikana, tumekagua na tumeridhika na uwekezaji huu na tunaiponegza PSSSF.” Amesema.

Amesema Kamati yake imeelekeza katika kipindi cha matarajio ya chumo la uwekezaji (Return of investment) inaleta tija na kupata chumo ndani ya muda iliyojiwekea kisha kuanza kupata faida.

“Na hii itakuwa ni faida kwa Mfuko na kuufanya uweze kuendelea kuwahudumia wananchama bila kutetereka.” Alisema.

Mwenyekiti huyo amempngeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna anavyosukuma mabadiliko ya kiuchumi nchini na uwekezaji huo umeakisi R mbili kati ya zile nne za Mhe. Rais ambazo ni Reforms na Rebuild.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Pius Chaya, licha ya kupongeza uwekezaji huo lakini pia ameishauri serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kuangalia uwezekano wa taasisi za umma ambazo ziko Dar Es Salaam kutumia jengo hilo.

“Hatuui taasisi binafasi lakini ipo haja ya kujaza nafasi zilizobaki.” Amefafanua Dkt. Chaya.

Akitoa wasifu wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru amesema jengo la PSSSF Commercial Complex ni jengo refu zaidi na ni moja ya alama za jiji la Dar Es Salaami, ni jengo refu sana katika nchi za Afriak Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Amesema jengo hilo lina minara mmitatu (towers) moja ni Commercial Complex ambalo ni refu zaidi lenye ghorofa 35 Executive tower lenye ghorofa 14 na eneo la maegesho lenye ghorofa 6.

“Hapa ndio panaitwa PSSSF Commercial Complex, kuna Executive tower ambako ni maalum kwa shughuli za maofisi, commercial complex linahusisha mabenki, ofisi mchanganyiko na kumbi za mikutano na shughuli nyingine za kijamii, lakini pia kuna ene la maegesho ya magari.” Amefafanua.

Amesema jengo hilo limeendelea kuwavutia wapangaji wengi zaidi kadiri muda unavyokwenda na matarajio ya Mfuko, kufikia desemba mwaka huu 2024, kiwango cha upangishaji kinatarajiwa kupanda na kufikia asilimia 70.

Amesema, miongoni mwa wapangaji mashuhuri kwenye jengo hilo ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP) na taasisi zake, kampuni kubwa ya mitandao ya simu Tigo, taasisi za umma, mabenki na wafanyabiashara binafsi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu, akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua mradi wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex, lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, Machi 21, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya PIC kukagua jengo, Machi 21, 2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima, akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam Machi 21, 2024.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), wakiongozwa NA Mwenyekiti wake Mhe. Deus Sangu na Menejimenti ya PSSSF wakitembelea jengo la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam Machi 21, 2024.

Mwenyekiti akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kwenye ghorofa lenye ofisi za UNDP

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipata maelezo kuhusu wapangaji wa jengo hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (Katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (Katikati), akimpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam Machi 21, 2024. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul-Razaq Badru.

Picha ya kumbukumbu baina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC) na Viongozi wa PSSSF.

Sehemu ya muonekano wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex, Barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam.
 
Majenereta ya usaidizi inapotokea umeme wa TANESCO umekatika.
Eneo la chini la maegesho ya magari
Bwawa la kuogelea eneo la Jengo la PSSSF Commercial Complex
Ngazi za umeme na za kawaida ndani ya jengo la PSSSF Commecial Complex

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages