LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 25, 2024

CHATANDA AMWAGA MAFANIKIO LUKUKI YA RAIS SAMIA, AKIFUNGUA MAFUNZO KWA MADIWANI WANAWAKE


 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT-Taifa), Mary Chatanda (katikati) akiwa na Kamisaa wa Sensa Tanzania, Anne Makinda (kulia) pamona na Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani wanawake kutoka  mikoa 11 kwenye Ukumbi wa Kilimani jijini Dodoma Machi 25, 2024.

Akizungumza katika mafunzo hayo amepata wasaa wa kuelezea mafanikio lukuki ya uongozi wa miaka mitatu ya  Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo ukamilishaji wa ujenzi wa Ikulu ya Dodoma, ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Daraja la Busisi Mwanza lililofikia asilimia 80, Bwawa la Mwalimu Nyerere, mradi wa mabasi ya mwendokasi (BRT) na mengine mengi.


Chatanda akisisitiza jambo

Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo akisema neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wake, Chatanda.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule akisema neno la ukaribisho mkoani humo kwa wajumbe wa mafunzo hayo.
Kamisaa wa Sensa Tanzania, Anne Makinda akihutubia wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi y madiwani na viongozi wananwake wakiwa katika mafunzo hayo.
Katibu wa wabunge wanawake wa CCM, Subira Mgalu akijitambulisha
Baadhi ya viongozi wa UWT Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa UWT wakiwa na bashasha walipokuwa wakitambulishwa.




IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA












No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages