Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Tegeta
BABA HALISI ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, leo Jumapili Machi 24, 2024 au (26 Abibu, 1 Majira Halisi), ametangaza jina jipya la Kanisa hilo kutoka Kanisa Halisi la Mungu Baba na kuwa Kanisa Halisi tu.
BABA HALISI ametangaza mabadiliko hayo, katika Mkutano Mkuu uliofanyika katika Ibada, iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, lango la 26 Abibu, 1 Majira Halisi.
Baada ya BABA HALISI kutangaza mabadiliko hayo ya jina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu huo kutoka vituo vya ndani na nje ya Tanzania wote waliunga mkono kwa kauli moja, kwa njia ya kila mmoja kutia saini katika fomu maalum, saini ikiambatana na picha ya mjumbe.
"Ni kweli kabisa leo tuna mawili, lakini ambayo yote ni moja, jambo kubwa ni Mkutano Mkuu wa Kanisa, lakini nitaanza na mafundisho mafupi ya Hatua kumi za Muumba akiwa anatafuta kanisa halisi. Hapo sasa utapata ufafanuzi kwa nini kunzia leo Kanisa litabadilika jina, Sasa jina litatoka kuwa refu na kuwa fupi, badala ya kusema Kanisa Halisi la Mungu Baba, tutasema Kanisa Halisi tu. Kwa hiyo wakati nafundisha nitatoa sababu kwa nini jina libadilike", akasema BABA HALISI.
Mapema kabla ya kuanza Ibada na Mkutano Mkuu huo, BABA HALISI alimuinua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Walio chini yake wote, tangu ngazi za juu hadi chini.
TAFADHALI MSIKILIZE BABA HALISI UPATE UHONDO WOTE. BOFYA HAPO👇👇
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇