Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua.
Taarifa iliyotolewa jana saa tatu usiku na Msemaji wa Familia Abdulkah Ali Mwinyi imesema baada ya Mzee Mwinyi kupelekwa Hospitali aliendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.
"Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali", amesema Abdullah Ali Mwinyi katika taarifa hiyo.
Mzee Ali Hassan Mwinyi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇