Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), Meja Jenerali Francis Mbindi akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma Februari 20,2024, kuhusu maandalizi hayo.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) ambao Tanzania ni mwenyeji.
Mkutano huo utakaoambatana na baadhi ya michezo pamoja na kutembelea baadhi ya vivutio nchini, unatarajiwa kuhudhuriwa na watu 300 kutoka nchi 140 wanachama wa Baraza hilo duniani.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma Februari 20, 2024, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo, Meja Jenerali Francis Mbindi amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam utaanza Mei 12, 2024 na uzinduzi utanywa na Rais Samia Mei 13, 2024.
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Meja Jenerali, Mbindi kuzungumza na vyombo vya habari.Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Michezo ya JWTZ, Kanali Martin Msumari akielezea kuhusu maendeleo ya michezo jeshini. Kushoto ni Meja Jenerali Mbindi.
Baadhi ya maafisa wa JWTZMkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akifafanua jambo.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇