Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Ubungo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya makubwa kuboresha sekta ya elimu katika Wilaya ya Ubungo, hivyo wanafunzi katika wilaya hiyo wanatakiwa kutilia mkazo masomo kama njia mojawapo ya kuonyesha shukurani zao kwa Rais Dk. Samia.
Amewataka wazazi na walezi nao kutowaacha huru watoto waosoma katika shule wilayani humo, badala yake wawafuatilie kwa karibu kuhakikisha kuwa watoto wao hao wanafika shuleni na kuzingatia masomo ipasavyo badala ya kuzurura na kufanya mambo ambayo yatawaharibia masomo na kufuta ndoto za baadaye.
Cde Mwajabu amesema hayo kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na Walimu, wanafunzi na Wazazi katika Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba iliyopo Kata ya Makuburi, na kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Jererali Mboma, Katika Kata ya Mabibo, ikiwa ni miongoni mwa shughuli zilizofanywa na UWT mkoa wa Dar es Salaam, kuadhimisha miaka 47 ya CCM.
“Najua kuna wazazi hapa, tusiache jukumu letu la kulea na kuwaacha walimu peke yao, watoto wetu hawataweza kutimiza ndoto za elimu katika maisha yao, naomba mtekeleze majukumu yenu ya msingi na kuwafuatilia watoto kila siku” akasema Cde Mwajabu
Katika Shule ya Yussuf Makamba Cde Mwajabu aliwataka wanafunzi wa kike na wa kiume kuacha kupoteza muda kwa kujishirikisha na masuala hatarishi kwa hatma ya maisha yao ya baadaye, akiwata wanafunzi wa kike kuachana na tamaa zinazowatumbukiza katika kutojali masomo na badala yake kukumbatia wanaume.
"Mambo haya kwa sasa hayawahusu, yawatapotezea muda, unacha masomo unaenda vichakani, mtu mwenyewe unayeenda nae hana uwezo wa kukutunza. angekuwa na uwezo asingekupeleka vichakanai. aka kabisa ujinga huu upatozewa muda, ukikosa majongwa unaibuka na mimba na hivyo utakuwa umeharibu hatma ya ndoto zako za maisha bora ya baadaye", akaonya Cde Mwajabu.
"Na ninyi watoto wa kiume msipozingatia masomo, na kuanza kuvuta bangi, kubwia unga mtatumbukia katika makundo maovu na hatimaye mtageuzwa mashoga. ukishakuwa shoga, umekwisha. Taifa hili linahitaji wanaume marijali wenye nguvu na uwezo wa kufanyakazi", Cde Mwajabu aliwanya watoto wa kiume.
"Mmeona hapa tumetoa bahasha zenye motisha kwa wanafunzi waliofanya vizuri kuanzia mwaka wa jana, Sasa mwaka huu naitaji mwaka huu wanafunzi zaidi ya 200 wa kidato cha nne mpate daraja la kwanza na bila shaka mkiamua hii linawezekana” akasema Cde Mwajabu.
Mwishoni mwa hafla hiyo Cde Mwajabu alichangia sh. Laki mbili (200,000) shule hiyo kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya kiada, kufuatia Mkuu wa shule hiyo Kane Kibangali kumweleza kwamba shule inakabiliwa na uhaba wa vitabu vya aina hiyo.
"Sasa hapa mimi nitatoa sh. laki mbili, lakini nataka mlete hapa kapu lenye kianzio, haya changishaneni huko kwanza", akasema Cde Mwajabu, na papo hapo ikapitishwa harambee huku na huko hazi zikapatikana zaidi ya sh. 50,000. ambazo maada ya kuchangaywa na za Cde Mwajabu zikafanya jumla ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitabu kufikia sh. 150,000.
Katika Mkutano wa UWT wa hadhara uliofanyika Kata ya Mabibo Cde Mwajabu aliwataka viongozi kuhakikisha wanajipanga vema ili CCM ipate ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu.
Aliwataka wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi, chini ya Mwenyekiti wake Rais Dk. Samia kwa sababu yaliyokwishafanywa na kuendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita yanaonekana. hivyo hakuna sababu ya kukinyima kura Chama Cha Mapinduzi.
"Serikali imefanya mengi katika Wilaya hii ya Ubungo, na kuna mengine hasa ya miundombinu yanaendelea kufanyika, ingawa kwa sasa ya miundombinu imesimama kidogo kutokana na mvua hizi ambazo zitaendelea hadi mwezi wa nne. Na suala la umeme kukatikatika lipo mbioni kufika ukingoni maana Bwawa la Mwalimu Nyerere litaanza kufanya kazi miezi michache ijayo, hivyo litawezesha umeme kupatikana muda wote.", akasema Cde Mwajabu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo akiwasili Shule ya Sekondari Yussuf Makamba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo akiwa na wenyeji wake kwenda kukagua madarasa mapya mwenye shule hiyo.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo akiwa na wenyeji wake kwenda kukagua madarasa mapya mwenye shule hiyo.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo akiwa na wenyeji wake kwenda kukagua madarasa mapya mwenye shule hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo, akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika chumba kipya katika shule hiyo ya Yussuf Makamba. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo, akizungumza na Wanafunzi na Walimu katika mkutano uliofanyika Shule ya Sekondari Yussuf Makamba, katika Kata ya Makuburi, Ubungo, leo Februari 2, 2024 ikiwa ni katika Maadhimisho ya UWT mkoa huo ya miaka 47 ya CCM. Wanafunzi Shule ya Sekondaroi Yussu Makamba wakimshangilia Cde Mwajabu Mbwambo.
Cde Mwajabu Mbwambo akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Yussuf Makamba waliofanya vizuri mwaka jana.
Wanafunzi waliofanya vizuri mwaka jana katika shule hiyo wakiwa mbele ya meza kuu baada ya kukabidhiwa zawadi zao na Cde Mwajabu Mbwambo.
Mkuu wa Shule hiyo akipokea mchango wa Sh. 250,00 kutoka kwa Cde Mwajabu Mbwambo, kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya kiada. katika fedha hizo Cde Mwajabu alichangia sh. 200,000.
Walimu wa shule hiyo wakiwa mbele ya meza kuu katika picha ya kumbukumbu.
Cde Mwajabu Mbwambo akiwa ameketi na Dada Mkuu wa Shule hiyo. pamoja naye ni Afisa Elimu na Afisa Mtendaji wote wa Kata ya Makuburi
Kwa pamoja wakasema; "Samia mitano tenaaaa. Kazi iendelee".
KATA YA MABIBO;
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo, akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Mkutano wa UWT uliofanyika Mtaa wa Jenerali Waitara, Kata ya Mabibo. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Ubungo Samina Mashauri.
Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Yvonne Fande akisalimia katika Mkutano wa UWT Kata ya Mambo. Vyonne pia ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UVCCM Kata hiyo.Diwani Kata ya Mabibo Joseph Kleruu akieleza Utekelezaji wa Ilani ya CCM ulivyofanyika katika Kata hiyo.
Diwani huyo akikabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Cde Mwajabu Mbwambo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Dar es Salaam Ashura Ng'onde akizungumza kwenye Mkutano huo wa kata ya Mabibo. Mwenyekiti wa UWT Ubungo Ashura Ng'onde, akimkaribisha Cde Mwajabu kuzungumza na Wana CCM na Wananchi kwa jumla kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Mwajabu Mbwambo, akizungumza na Wana CCM hususan UWT katika mkutano wa UWT uliofanyika Kata ya Mabibo, leo Februari 2, 2024 ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 47 ya CCM.Cde Mwajabu Mbwambo akigawa kati ya UWT kwa Mmoja wa wanachama wapya 110 waliojinga na Jumuiya hiyo.
Cde Mwajabu Mbwambo akigawa kati ya UWT kwa Mmoja wa wanachama wapya 110 waliojinga na Jumuiya hiyo.
Cde Mwajabu Mbwambo akigawa kati ya UWT kwa Mmoja wa wanachama wapya 110 waliojinga na Jumuiya hiyo.
Cde Mwajabu Mbwambo akigawa kati ya UWT kwa Mmoja wa wanachama wapya 110 waliojinga na Jumuiya hiyo.
Cde Mwajabu Mbwambo akigawa kati ya UWT kwa Mmoja wa wanachama wapya 110 waliojinga na Jumuiya hiyo.
Baadhi ya Wanachama wapya wa UWT wakionyesha kadi zao baada ya kukabidhiwa na Cde Mwajabu Mbwambo.
UWT Kata ya Mabibo wakimtuza Cde Mwajabu Mbwambo.
Cde Mwajabu Mbwambo akishirikiana na Havinitishi na Ashura Ng'onde, kukata keki ya 'HAPPY BIRTHDAY CCM'Kisha Cde Mwajabu akamlisha Mwenyekiti Ng'nde
Halafu akamlisha Havinitishi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇