Na Mwandishi Maalum, Arusha
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Arusha Timoth Sanga, amesema Chama kwa kushirikiana na seriali katika Wilaya hiyo, kitaendelea kusikiliza na kutatua changamoto katika sekta mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Sanga amesema hayo jana wakati wa mwendelezo wa ziara ya mtaa kwa mtaa ya sekretarieti ya CCM wilaya ya Arusha yenye lengo la kusikiliza na utatua kero zinazowakabili wananchi katika kata ya Murieti iliyopo Jijini Arusha.
“Niwaombe sana wananchi wa Kata ya Murieti, tuendelee kujenga imani na CCM kwa sababu ndiyo yenye Serikali. Nataka niwahakikishie kwamba changamoto zote zinazowakabili katika sekta mbalimbali kwenye kata hii tutazifanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali”
Kutokana na changamoto ya miuondombinu mibovu ya barabara katika kata hiyo ikiwemo kivuko cha Sojema kilicho mtaa wa Murieti katika kata hiyo ya Murieti Sanga alilazimika kumpigia simu ya kiganjani meneja wa Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA) mhandisi Kyando ambaye alikiri kufahamu changamoto ya kivuko na baadhi ya barabara za kata hiyo.
“Katibu ni kweli kuna changamoto ya kivuko cha Sojemba ambacho kinaleta adha kubwa kwa wananchi wa eneo hilo na hii inatokana na halmashauri ya Jiji la Arusha kuwa na malipo mengi ya fidia hali inayosababisha kushindwa kumlipa mmoja wa wananchi fidia ili tutengeneze barabara hiyo pamoja na kivuko”.
“Lakini naomba nikuahidi Januari 15 mwaka huu tutakwenda tena eneo hilo kwa ajili ya kuona namna bora ya kujenga kivuko cha gharama nafuu ili magari yaweze kupita eneo hilo na wananchi wapate huduma za usafiri”.
Awali akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Fracis Paschal amesema wananchi walichangishwa fedha pamoja na kuelekezwa wavunje nyumba zao bila fidia kupisha ujenzi wa barabara na kivuko lakini hadi sasa ni miaka kadha hakuna kilichofanyika.
“Changomoto kubwa inayotukabili katika eneo hili ni kivuko pamoja na barabara ambapo uongozi wa kata ukiongozwa na diwani tulichangishwa fedha za kumlipa mmoja wa wananchi fidia ili kupisha ujenzi na wengine tulibomoa nyumba zetu bila fidia lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea”
Kwa mujibu wa Paschal kauli za serikali kupitia wakala wa barabara za Mijini na Vijiini (TARURA) wilaya ya Arusha hazitekelezeki tunawaomba viongozi wa CCM ngazi ya wilaya mtusadiei changamoto hii kwa sababu imekuwa kero kubwa na watendaji hawa wanaichonganisha serikali na wananchi pamoja na CCM”.
Diwani wa wa kata ya Murieti Fracis Mbise alikiri uwepo wa changamoto ya kivuko cha Sojema hali inayosababisha wananchi kushindwa kuvuka eneo hilo mvua zikinyesha pamoja na wanafunzi huku akieleza kuwa ameshawasiliana na TARURA wilaya ya Arusha bila mafanikio mara kadhaa.
“Mvua zikinyesha wananchi baadhi ya wananchi wanashindwa kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali wakiwemo wanafunzi lakini pia kuna mama alishajifungulia hapa kutokana na changamoto ya kivuko na nilimchukua kumpeleka hosptali akiwa na mtoto tayari”.
Katika ziara hiyo iliyoongizwa na Sanga wajumbe wa sekretarieti ya wilaya wasikiliza kero mbalimbali zikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara,vivuko,elimu,afya na ukosefu wa mitaji kwa mama ntilie pamoja na vikundi vya waendesha bodaboda.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha Timoth Sanga, akizungumza na Diwani wa Kata ya Murieti Francis Mbise (kulia) wakati wa ziara ya mtaa wa mtaa ya Sekretarieti ya CCM wilaya hiyo, kusikiliza kero zinazowakabili wananchi katika kata hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Arusha Timoth Sanga, akizungumza na wananchi eneo la kivuko cha Sojema, baada ya kujionea hali ya miundombinu ya barabara katika eneo hilo, wakati wa ziara ya mtaa wa mtaa ya Sekretarieti ya CCM wilaya hiyo, kusikiliza kero zinazowakabili wananchi katika kata ya Murieti iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Arusha Timoth Sanga aitangulia kuvuka mfereji eneo la Sojema wakati akiwa katika ziara ya Sekretarieti ya CCM katika wilaya hiyo kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Murieti iliyopo Halmashauri ya Jiji la Arusha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇