LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 15, 2024

CCM DMV MAREKANI WAMPONGEZA BALOZI DK. NCHIMBI KUWA KATIBU MKUU WA CCM, WASEMA WANAIMANI ATAKIVUSHA CHAMA, NI MZOEFU, MCHAPAKAZI

CCM DMV, Marekani
Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Tawi la Washington DC, Maryland na Virginia (DMV) Salma Moshi, kwa niaba ya Wanachama wenzake, amempongeza Balozi Mstaafu Dk. Emmanuel Nchimbi kwa kuwa Katibu Muu wa CCM.

Katika salamu alizozituma Blog ya Taifa ya CCM, Salma ameeleza kuwa yeye na wanachama wenzake wana matumaini kwamba Dk. Nchimbi ataleta chachu kubwa katika chama kwa kuwa ni mzoefu katika CCM kwa muda mrefu, mwaminifu na mchapakazi.

"Kwa niaba yangu na wanachama wa CCM tawi la DMV nampongeza Ndugu Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, mimi na wenzangu tunaamini ataleta chachu kubwa katika Chama. CCM OYEEEE!", ameandika Salma katika salam hizo.

Balozi Dk. Nchimbi ameteuliwa na Kamati Kuu Maalum ya CCM na baadaye uchaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, katika vikao vya Kamati Kuu Maalum na NEC vilivyofanyika mjini Zanzibar, chini ya Mwenyeiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 15, 2024.

Balozi Dk. Nchimbi akiwa na Kiongozi wa CCM Tawi la MDV, Mareani Salma Moshi. (Picha na Maktaba).
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages