Mbezi, Dar es Salaam
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda , Disemba 21, 2023, alimkabidhi mchango wake binafsi wa Sh. milioni 10, aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Mwanamuziki wa muziki wa kiazazi kipya (HipHop) nchini Joseph Haule Maarufu Profesa Jay.
Alimkabidhi fedha hizo alipofika nyumbani kwake (Profesa Jay) Mbezi Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kutimiza ahadi yake, ambapo pia alimkabidhi kiasi kingine cha Sh. Milioni 10 ambacho Mwenezi Makonda alisema ni mchango kutoka kwa Ndugu yake, hivyo akawa amemkabidhi jumloa ya sh. milioni 20.
Pamoja na kumkabidhi fedha hizo, Mwenezi Makonda alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha walioahidi kutoa michango yao kwa kuwa ahadi ni deni, huku akimuomba Profesa Jay kumpatia orodha ya walioahidi ili amsaidie kuwafuatilia.
Pia Mwenezi Makonda alimuahidi Profesa Jay kumtafutia nyumba eneo la karibu na hospitali ya Muhimbili anakopatiwa matibabu ili kupunguza changamoto ya umbali wa kutoka anakoishi Mbezi kwenda kupatiwa matibabu.
Mwenezi Makonda alitoa ahadi yake binafsi kumchangia fedha hizo Profesa Jay wakati wa uzinduzi wa Professor Jay Foundation uliofanyika Jijini Dar es Salaam,Disema 20, 2023, ili kupeleka tabasamu na kusaidia wagonjwa wa figo nchini.
Akizunguma, Profesa Jay alimshukuru Mwenezi Makonda lakini pia akamweleza changamoto ya umbali unaomkabili kutoka Mbezi hadi kufika Hospitali ya Muhimbili kupatiwa matibabu, ndipo Mwenezi Makonda akamuahidi kumtafutia nyumba ya kumpangishia maeneo kama Upanga au Magomeni ambayo ni karibu na Muhimbili kuaepusha changamoto hiyo ya umbali.
TAZAMA MWENEZI MAKONDA ALIPOFIKA NYUMBANI KWA PRPFESA JAY👇








No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇