LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 23, 2023

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AWAPA SHANGWE YA KRISMAS NA MWAKA MPYA YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

Kimara, Dar es Salaam
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango leo amekabidhi zawadi ambazo ni pamoja na vyakula, vinywaji, sabuni, mafuta ya kupikia na mavazi, katika Kituo cha kulea watoto yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi zawadi hizo Msaidizi wa Makamu wa Rais masuala ya Sheria Elisha Suku amesema Makamu wa Rais ametoa zawadi hizo kusheherekea pamoja na watoto hao sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, huku akiwatakia heri na afya njema watoto pamoja na walezi wao.

Akipokea zawadi hizo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la KilutheriTanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es Salaam Wilbroad Matsai amemshukuru Makamu wa Rais kwa zawadi hizo pamoja na viongozi wote wanaojitolea kusaidia wenye uhitaji.

Msaidizi wa Makamu wa Rais masuala ya Sheria Elisha Suku (mwenyeko tijeusi) akikabidhi zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, katika Kituo cha kulea watoto yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam, leo Disemba 23, 2023 Watatu kutoka kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la KilutheriTanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Wilbroad Matsai.
Baadhi ya zawadi mbalimbali alizotoa Makamu wa Rais Dk.Mpango kuwapatia watoto hao yatima.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages