Hanang, Manyara
Wizara ya Afya kwa kushirikiana Shirika la Save the Children imetoa Mafunzo kwa Walimu apatao 30 ya kuwajengea uwezo wa kutoa msaada wa kisaikolojia shuleni, miongoni mwa mafunzo hayo wakiambiwa haipaswi kumzuia kulia anapopatwa na changamoto kwa kuwa kulia husaidia kumrejesha mtu huyo katika hali ya kawaida asijizuru.
"Baada ya janga hili watu wengi waliumizwa hivyo wanapolia kuonesha hisia zao tuache walie ila tuwasaidie kurejea katika hali yao ya kawaida na pia mtu anayetaka kujiua tunaomba haraka tuwasiliane kwa ajili ya msaada wa Kisaikolojia na watu wanaotumia pombe kama sehemu ya kukabiliana na changamoto hii ya mafuriko yaliyotokea Hanang ni muhimu pia kutoa taarifa ili kumsaidia huduma za Kisaikolojia, amesema Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasiyoambukiza, Afya ya Akili na Ajali kutoka Wizara ya Afya Dk. Omary Ubuguyu.
Akizungumza baada ya kutolewa mafunzo hayo Mjini Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara, Dk. Ubuguyu amesema mafunzo hayo yatasaidia walimu kuweza kutoa huduma za Kisaikolojia kwao binafsi na watoto watakapofungua shule.
“Mafunzo haya yatasaidia sana walimu kuwa na uwezo wa kutoa huduma ya Kisaikolojia na kama serikali imeanzisha Programu maalum ya “Back to School Proramme kwa sababu baada ya janga hili, tunatarajia kufungua shule mwezi Januari na watoto wengi watakuwa wamerudi shuleni na kwa bahati mbaya wapo watoto ambao tumewapoteza au kupoteza ndugu kwa hiyo kabla ya kufika Januari tumeanza kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwa na uwezo wa kutoa msaada ya Kisaikolojia”amesema.
Baadhi ya Walimu kutoka katika kata zilizoathirika na mafuriko Wilayani Hanang Mkoani Manyara wamesema mafunzo ya Saikolojia waliyopata kutoka kwa Watalaam kutoka Wizara ya Afya yatawasaidia kuwaweka katika hali ya kawaida wanafunzi
“Mafunzo haya yatatusaidia kukaa vizuri na wanafunzi na namna ya kuwajenga Kisaikolojia maana unakuta mwanafunzi alikuwa na wazazi ama walezi wake lakini atakapofungua shule utakuta hana rafiki aliyekuwa anakaa naye karibu hivyo mafunzo haya yana umuhimu sana kwetu” wamesema kwa nyakati tofauti.
Dk. Omary Ubuguyu.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇