Na Lydia Lugakila, Misenyi.
KATIBU tawala wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera Mwanaidi Mohamed Mang'uro amepongeza sherehe za maadhimisho ya maendeleo ya kata ya Kanyigo kwa mwaka 2023 zilizofanyika katika kijiji cha Kikukwe maarufu -KIKUKWE DAY wilayani Misenyi Mkoani Kagera Disemba 27,2023 katika Uwanja wa shule ya sekondari kikukwe.
Mwanaidi amesema kijiji hicho kumempa faraja kubwa baada ya kuunda umoja wa maendeleo unaofahamika kwa jina la moja wa maendeleo Kikukwe -UMKI ambao unaoonekana kuleta maendeleo makubwa katika kijijini hapo huku akiviomba vijiji vingine kuiga mfano kupitia kijiji hicho.
Katibu tawala huyo amewapongeza Wanakijiji hicho kwa kufanya maendeleo makubwa ikiwemo kushiriki ujenzi wa zahanati ya kata, kuleta walimu wa ziada katika shule nne za kijiji hicho na kuleta maji katika shule ya sekondari Kikukwe ambapo aliahidi kushiriki kikamilifu katika mipango yote ya maendeleo kwa mwaka 2024.
Naye Katibu wa umoja huo Bi Magreth Domisian alitaja kazi mbalimbali zilizofanywa na umoja huo ambazo zilimfurahisha Katibu tawala, kuwa mwaka 2023 umoja huo ulichangia katika shughuli za ujenzi wa kituo cha afya cha kata Kanyigo, kuweka maji, kujenga Bweni la Wasichana na kutoa mashine za kudurufu nakala za mitihani katika shule ya sekondari ya Kikukwe, na kuleta Walimu wa ziada katika shule nne kijijijni hapo.
Aidha kijiji hicho kimeanzisha kilimo cha Parachichi, Vanilla pamoja na ndizi ambapo wameendaa Darasa la kilimo ili Wanakijiji wapate Elimu ya kutosha kuhusu kilimo hicho.
Bi Magreth Ameongeza kwa mwaka 2024 wana mipango mingi ya ikiwemo kujenga maktaba, kumbi mbalimbali na ujenzi wa maduka ya jumla na mradi wa ujenzi tayari umenza lakini pia watawezesha michezo kwa wanafunzi pamoja kuendelea kuchangia katika kuwawezesha Wanafunzi katika Elimu kwa kutoa vitendea kazi kama vitabu na Walimu katika shule za kijiji hicho.
Aidha Mwenyekiti mhandisi Godfrey Mugini wa umoja wa huo amejivunia kuwa mmoja wa wanakijiji hicho kwani matarajio yao ni kijiji kuwa cha mfano wa kuigwa kwa vijiji vingine huku akiiomba Serikali kutatua baadhi ya changamoto walizonazo ikiwemo miundo mbinu mibovu kama Barabara ya kutoka Gera kwenda mpakani mwa Uganda pamoja na uhitaji wa fedha ili kutimiza malengo ya umoja huo.
Naye Diwani wa kata ya Kanyigo amewapongeza wanakijiji hao kwani wamekuwa mfano mzuri kwa vijiji vingine kwenye kata hiyo huku akiahidi kupambana ili changamoto zinazojitokea zitatuliwe ili wanakijiji hao wafikie malengo yao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇