Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Maafa UWT na Viongozi wa Mikoa ya Manyara na Arusha leo Disemba 05, 2023 wamefika kuwajulia hali Majeruhi wa Maafa ya Mafuriko yaliyosababisha kuporomoka kwa tope na Mawe kutoka Mlima Hanang, Katesh Mkoani Manyara.
MCC Chatanda amesema Majeruhi hao wanapatiwa matibabu bure na Serikali katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara na Sisi kama Umoja wa wanawake Tanzania UWT tumeona tuje tuwaone wananchi wetu wa Hanang kwa kuja kuwafariji kwa kidogo ambacho kama UWT tumekipata na tutaendelea kuleta Misaada mbalimbali kwenu ili iweze kuwasaidia .
UWT IMARA JESHI LA MAMA SAMIA KAZI IENDELEE.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇