Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Cde Mwajabu Mbwambo, amesema 'Uchaguzi ni namba' hivyo ili kujihakikishia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa (2024) na Uchaguzi Mkuu (2025) ni lazima Jumuiya hiyo na CCM kuwa na wanachama wengi iwezekanavyo.
Cde Mwajabu Mbwambo ameyasema hayo katika mkutano wa ndani wa UWT tawi la Kivule Mashariki, na kusisitiza kwa Kivule ni lazima wafanye jitihada za kuongeza wananchama kwa kuwa kulingana na sensa ya watu na makazi iliyopita, Kivule ina wakazi wengi, lakini pamoja na wakazi hao kuwa wengi Idadi ya wananchama wa CCM na UWT kwenye tawi hilo ni ndogo.
Aidha Cde Mwajabu Mbwambo amesisitiza wanawake wa makundi ya rika mbalimbali kujitoa kwa wingi muda ukifika kuingia katika kuwania nafasi za uongozi 2024/2025, sanjari na hilo akiwakumbusha viongozi wa kata na ngazi zingine za uongozi kushusha chini Mafunzo waliyopewa tarehe10/06/2023 na UWT Mkoa katika matawi yote ya UWT Mkoa wa Dar es salaam, kwa kuwa kuna baadhi ya matawi ambayo wamekiri mafunzo hayajawafikia hivyo kutokuwa na uelewa na baadhi ya mambo na kuhitaji kujengewa maarifa.
Cde Mwajabu Mbwambo alipongeza tawi hilo kwa kuandaa jambo la kumpa hamasa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake katika eneo la kivule Mashariki, ikiwa ni pamoja na kupewa fedha za Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari na msingi.
Pia amewapongeza kwa ushirikiano mkubwa waliokuwa nao katika chama na nje ya chama ambao unaleta mshikamano mkubwa na ushirikiano katoka mambo mbalimbali ikiwemo wananchi kuweka nguvu zao kujenga baadhi ya vivuko katika barabara
Cde Mbwambo alisema anaijua changamoto ya barabara za kivule na maeneo mengine ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, akasema Mamlaka za barabara TARURA zitafanya ukarabati baada ya Mvua zinazoendelea kunyesha zikikoma.
Kuhusu suala la mikopo ya asilimia 10 ambalo Wanawake wa UWT Kivule Mashariki walikumbushia na kuhitaji ufafanuzi Cde Mwajabu Mbwambo aliwakumbusha kwa sasa utaratibu umebadilika ni lazima kikundi kusajiliwa kwenye mfumo, na serikali imeandaa mpango mzuri wa kutoa mikopo hiyo na amekumbusha kwa wadaiwa sugu wa mikopo wahakikishe wanalipa ili wengine kunufaika na mikopo hiyo isiyo na riba.
Cde Mwajabu Mbwambo pia amewaasa viongozi wa UWT Kuhakikisha wanasimamia na kuwa mabalozi wazuri katika kupambana na ukatili wa kijinsia na baadhi ya wanawake kuacha kunyanyasa waume zao baada ya kupata uongozi na kuwa na kipato kikubwa kuliko mume.
Amehiza kua katika suala la Malezi na Maadili kwa watoto Mama ndio Mwalimu na mlezi Mkuu wa familia hivyo pamoja na kuwa viongozi bado asili ya uumbaji tutabakia kuwa walezi bora ili kujiepusha na mporomoko wa maadili kwa watoto wetu katika jamii ya kivule na taifa kwa ujumla.
Amekumbusha na kukazia suala la Siasa na Uchumi Tawi hilo lijipange kuwa na mradi wake ili kusimama imara katika kuhakikisha Uwt inasonga mbele na kuhitimisha kwa kuwataka wanawake kupendana , kusaidiana, kuelimishana, kuacha vinyongo, unafiki na kutengenezeana majungu kwani Adui wa mwananamke si mwanamke bali ni tabia za mtu binafsi alizonazo katika kuharibia wengine hivyo "tudumishe upendo na kuwa na hofu ya mungu".
![]() |
| Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Cde Mwajabu Mbwambo, akizunumza katika Mkutano wa ndani na UWT tawi la Kivule Mashariki. |
![]() |
| Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Cde Mwajabu Mbwambo, akizindua Shina namba 1 la Wakeeketwa wa tawi la UWT Kivule. |
![]() |
| Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Cde Mwajabu Mbwambo, akipandisha bendera kwenye Shina la Wakeeketwa wa tawi la UWT Kivule. |







No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇