LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 6, 2023

ALIYEJIFUNGUA SALAMA BAADA YA KUNUSURIKA MAFURIKO HANANG AMLIZA CHATANDA

 




 

Mwenyekiti  wa Umoja wa wanawake  Tanzania UWT, Mary Chatanda  na msafara alioambata nao wamejikuta katika Simanzi nzito mara baada ya kumuona  Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope ambalo lilikuwa limemuonea mwili mzima na kumsomba mita kadhaa.


Akizungumza leo alipomtembelea Mwanamke huyo katika  Kituo cha Afya Gendabi mahali  ambapo ndipo kulikuwa  na Maafa makubwa kufuatia mafuriko yaliyotokea mara baada  ya Mlima Hanang kupasuka.

"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama  huyu ambaye  alisombwa na tope na kuweza kuokolewa kwenye tope hilo  na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua  salama

Mtoto wa kiume 3/12/2023 kwa kweli nimelia uchungu baada ya kusikiliza simulizi za Mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku mjamzito wa miezi tisa hakika hakuna kama Mama . Namshukuru sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha Mama huyu kujifungua salama na mtoto yupo Salama na ameitwa Mussa ." 


Aidha Mwenyekiti  amesema  Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea mahitaji ya kutosha 

Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang . 


UWT IMARA JESHI LA MAMA SAMIA KAZI IENDELEE.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages