LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 11, 2023

WAUUGUZI WATARAJALI WAHITIMU MAFUNZO HOSPITALI YA TEMEKE

Na Cleopatra Mokiwa, Afisa Uhusiano, Temeke Regional Referral Hospital
Wauuguzi Watarajali 14 wamehitimu mafunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke na kuagwa rasmi na kupatiwa vyeti vya kuhitimu, katika hafla iliyofanyika kwenye Hospitali hiyo, jana, huku wakiaswa kuendeleza juhudi zao katika utoaji wa huduma bora za afya na kuwa watoa huduma wenye upendo kwa kila mgonjwa watakayemhudumia.

Pamoja na kuwaasa, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Joseph Kimaro, amewapa hongera za dhati wahitimu kwa mafanikio waliyopata na pia kuwataka kufuata taratibu na viapo vya uuguzi wanapotekeleza majukumu yao.

Amewasisitiza umuhimu wa kuwa wauuguzi wenye uadilifu, watiifu, na kujituma katika kutoa huduma kwa jamii. Aidha amewataka watarajali hao kuweza kutumia muda wao kujifunza mambo mapya nakuendelea kupata elimu zaidi ili kuweza kutoa huduma bora ya afya.

Nae, Muuguzi Mfawidhi, Nuswe Ambokile amewataka wahitimu hao kuheshimu miongozo ya maadili ya uuguzi na kuwa wachapakazi na waadilifu, Amewataka kufanya kazi kwa usawa na haki, bila kujali hali ya mgonjwa, na kutoa huduma kwa upendo na utu.

Mmoja wa wahitimu Halima Mohammed, amesema amejifunza mambo  mengi mazuri na ameahidi kwenda kuyatenda mambo aliyojifunza huko anapokwenda kufanya kazi.

Pia amesema kuwa mwanzo aliogopa kuja lakini baada ya kufika na kufanyakazi Temeke ameona yanayo ongelewa kuhusu Temeke sio kweli  kwani ina wataalamu walio na moyo wa kujitoa kwaajili ya wagonjwa wao.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Joseph Kimaro.
Muuguzi Mfawidhi, Nuswe Ambokile.
Wauuguzi Watarajali.
Wauuguzi Watarajali.
Wauuguzi Watarajali.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages