LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 17, 2023

MWAJABU MBWAMBO ATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU ACHAGULIWE KUWA MWENYEKITI WA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM, ATUMA SALAM ZA SHUKURANI KILA KONA

Official CCM Blog, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, C'de Mwajabu Rajabu Mbwambo leo Novemba 17, 2023 ametimiza mwaka mmoja tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo Novemba 17, 2022.

Kufuatia baraka hiyo, amemhsukuru Mwenyezi Mungu na kutuma salam za shukurani kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT mkoa huo, Viongozi na Wanachama, wapenzi wa UWT, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya zingine na Wanawake wote wa mkoa wa Dar es Salaam kwa jumla.

"Habari ndugu wajumbe wa mkutano mkuu UWT Mkoa, viongozi na wanachama, wapenzi wa UWT, CCM,  Jumuiya zingine na wanawake wote kwa ujumla wa mkoa wa
Dar es salaam.

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutimiza mwaka mmoja (1) katika jukumu mlilonikabidhi
Tarehe kama ya leo 17/11/2022, kwa mapenzi yenu makubwa sana mliniamini na kunipa dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es salaam.

Nawashukuru sana kwa Dua na sala zenu, umoja, mshikamano, ushirikiano na mapenzi makubwa mlionipa, kwa pamoja tumeweza kufanikisha mengi ndani ya jumuiya yetu katika mkoa wa Dar es salaam, ikiwa ni pamoja na uhai wa jumuiya kufanyika kwa vikao vya kikatiba ngazi zote za uongozi kuanzia tawi, kata wilaya na mkoa, kufanyika kwa ziara za kikazi na kukagua utekelezaji wa ilani, mafunzo mbalimbali ya uongozi na mengineyo.  

Tumeweza kuimarisha ushirikiano mzuri wa UWT na serikali na asasi zisizo za serikali ndani ya mkoa, UWT Kuwa mstari wa mbele katika kusaidia makundi yenye uhitaji katika ngazi zote za uongozi, tawi, kata wilaya na mkoa, Mapokezi ya viongozi mbalimbali, na kufanyika kwa makongamano na pia kushiriki katika shughuli nyingi mbalimbali katika jamii.

Nawashukuru sana sina cha kuwalipa zaidi ya kuombeana dua kwa Muumba wa mbingu na ardhi ili kila mmoja wetu atimize ndoto na malengo yake yenye manufaa makubwa kwa UWT na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

Kipekee naishukuru CCM kwa kuendelea kulea Jumuiya ya UWT katika ngazi zote za uongozi kwa maelekezo, miongozo na mafunzo.

Nawapenda sana, tuzidi kudumisha upendo na mshikamano wetu na kuwa juimuya ya kuigwa. Na tuweze kufanikiwa kupata ushindi wa kishindo kwa chaguzi zijazo na wanawake wajitokeze kwa wingi katika kuwania nafasi za uongozi.

Muumba awahifadhi na kuwalinda na awabariki sana", ameandika Mwajabu Rajabu Mbwambo, katika salam hizo ambazo Blog ya Taifa ya CCM imepata nakala ya andiko lake, akihitimisha kwa kuandika "Kidumu Chama Cha Mapinduzi, UWT Imara, Jeshi la Mama, Kazi Iendelee.

Mwajabu Raiabu Mwambo

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages