LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 17, 2023

CHONGOLO AMPONGEZA PROFESA J KWA UAMUZI WA KISHUJAA


 "Nimepata muda wa kutafakari juu ya maisha. Nikatumia muda mwingi kuyafikiria mapito aliyopitia rafiki yangu Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa J." 

"Mwaka jana nilipata wasaa wa kumtembelea Prof. J hospitali Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Baada ya miezi mingi na siku tele kupita Mungu akatuletea funzo kupitia yeye kwa kumpa uponyaji na kumfanya aungane nasi tena katika maisha huru."

 "Haikuwa rahisi kwake lakini zaidi kwa familia yake hasa mkewe. Wiki iliyopita Profesa J alitembelea Bunge ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha na kuitangaza taasisi aliyoianzisha."

 "Lakini pia amefanikiwa kutoa wimbo wenye funzo kubwa kwetu. Kinachonivutia na kilichonihamasisha kuandika katika ukurasa wangu huu ni namna Profesa J alivyobeba moyo wa huruma dhidi ya wagonjwa wanaopitia changamoto za figo nchini tatizo lililomsumbua sana yeye na kuona haja ya kutafuta namna ya kushiriki kwa kutafuta chochote kuchangia jitihada za serikali katika kuokoa maisha ya wanaopitia changamoto hiyo."

"Hakika nimeguswa, na nitafanya jambo, ila nimeona sadaka yangu kubwa iwe kuhamasisha wengine kuguswa na dhamira ya ndugu yetu." 

"Na kwa namna moja au nyingine iwe kupitia kwake au moja kwa moja kushiriki kwa tulivyojaliwa kuwatembelea wagonjwa na kushiriki kurejesha furaha kwao."

"Pole Profesa J. Hongera kwa uamuzi huo wa kishujaa."

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages