LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 31, 2023

RAIS WA UJERUMANI NDANI YA TANZANIA, LEO, OKTOBA 31, 2023


Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akipunga mkono mara baada ya kuwasili nchini. Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba akimpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimian Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani Mhe. Thomas Terstegen alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikabidhiwa maua alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier  wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta kwenye hafla ya mapokezi ya Rais huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages