Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) kupitia Mkoa wa Rukwa, Sultan Saleh Seif ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia Mkoa wa Rukwa Fedha lukuki za miradi ya maendeleo Mkoa wa Rukwa.
Aidha ameiomba serikali kuupatia mkoa huo madaktari bingwa kutokana na upungufu mkubwa uliopop wa madakatari hao.
Ametoa shurani hizo na maombi hayo wakati wa mkutano wa kuhitimisha ziara ya siku nne ya Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo mkoani humo kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga Oktoba 11, 2023.
Ziara hiyo ya Chongolo ambaye aliambatana na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ilikuwa ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇