![]() |
Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya KCB, Christina Manyenye (kushoto) akimkabidhi madawati 120 Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, ndugu Silvestry (kulia). Nyuma ya Christina ni Mwl. Mwajuma Nyamka, Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini na nyuma ya ndugu Koka ni Mkurugenzi wa Kibaha Mjini Mshamu Munde (anayepiga makofi).Mbunge wa Kibaha Mjini leo 12/10/2023 amepokea na kugawa Madawati 120 yaliyotolewa na KCB Benki. Ujio wa Madawati hayo ni Matokeo ya Maombi ya ndugu Silvestry Koka aliyoomba mapema Julai mwaka huu. |
Akikabidhi Madawati hayo, kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa KCB, ndugu Christina Manyenye (kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko amesema Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanachangia shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na majanga.
“Kutoa Madawati hayo ni matokeo ya ushirikiano mkubwa kati ya ndugu Koka na Benki hiyo kama mdau muhimu,” ameeleza Christina.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kibaha Mjini, ndugu Christina ameeleza pia kuwa madawati hayo ni moja ya madawati imara sana kwa kuwa yametengenezwa kwa mbao ngumu za mninga na yamegharimu pesa nyingi hivyo ametoa rai yatunzwe vyema.
Akipokea madawati hayo ndugu Koka ameishukuru KCB Benki pamoja na menejimenti yake na kuongeza kuwa madawati hayo atayagawa kwa shule ya Msingi Mkuza 40, Shule ya Msingi Maendeleo 20, Shule ya Msingi Miembesaba 20, Shule ya Msingi Kidimu 20 pamoja na Shule ya Msingi Kambarage 20.
Akitoa Salamu za shukrani, Mwenyekiti wa CCM wilaya Mwl. Mwajuma Nyamka amesema viongozi wa chama wamefika katika hafla hiyo kushuhudia na kumuunga mkono ndugu Koka kwa namna anavyotekeleza ilani aliyokabidhiwa.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇