Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Chongolo (kushoto) akikagua Ujenzi wa Shule ya kisasa ya sekondari ya Kata ya Inyonga wilayani Mlele mkoani Katavi Oktoba 5, 2023 wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Chongolo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Mlele kwa kusimamia vizuri ujenzi wa shule hiyo ya kisasa.Mradi huo ulianza Agosti 4, 2023 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 31, 2023 na itaanza kuchukua wanafunzi Januari mwakani.Shule hiyo ikikamilika itaitwa Mlele.
Shule hiyo inayojengwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari Tanzania (SEQUIP) imepokea zaidi ya sh. mil. 600 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Chongolo akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇