LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2023

WAZIRI MAJALIWA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI KAGERA


 

Na Lydia Lugakila,

Bukoba.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  amefunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Mkoa wa Kagera huku akiwataka viongozi kuonesha matokeo chanya yatakayo wanufaisha wananchi kwa haraka kupitia mikakati mbali mbali ya kimaendeleo.


Waziri Majaliwa Alitoa kauli hiyo Septemba 22, 2023 katika ukumbi wa ELCT uliopo Manispaa ya  Bukoba Mkoani Kagera wakati akifunga  mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao wa Mkoa yaliyoandaliwa  na Taasisi ya uongozi ambapo aliwataka viongozi kuimarisha mahusiano katika

maeneo yao ya kazi, na kuweka mikakati ili Serikali ione matokeo chanya yatakayo wanufaisha wananchi kwa haraka ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.


Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Samia ameendelea kuwa mfano mzuri katika kuwajali Watanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo hivyo ni wajibu wa viongozi  wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha  wananchi wanapata maendeleo.


"Viongozi wote wa Halmashauri Hakikisheni mnawatumikia zaidi Wananchi, mkamsikilize kero zao na kuzitatua wafikieni msisubiri waje maofisini kwenu"alisema Waziri Mkuu.


Ameongeza kuwa Viongozi hao wanapaswa kufanya kazi kwa uaminifu hasa katika upande wa fedha inayoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema miradi hiyo.


Aidha amehimiza kila Kiongozi kuhakikisha  anasimamia matumizi ya fedha za Serikali kwani fedha hizi ni kodi za wananchi ni lazima zikatekeleze miradi ya maendeleo katika viwango na kufanya ufuatiliaji kwa kila mradi ili kuwa katika hali iliyokusudiwa.


Hata hivyo Waziri Majaliwa anaanza ziara ya kikazi mkoani Kagera mnamo Septemba 23,2023.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages