LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 28, 2023

MSD YAMSHUKURU RAIS DK. SAMIA KUIVUSHA, HALI YA UPATIKANAJI BIDHAA ZA AFYA YAONGEZEKA HADI ASILIMIA 64 KUTOKA 51

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog, Dar es Salaam
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ikisema imenawiri kiutendaji kutokana na kuivusha kupitia Serikali ya Awamu ya Sita anayoingoza, kwa kuipatia fedha za kutosha tena kwa wakati na hivyo kuweza kutekeleza majukumu na mipango yake vizuri.
 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Ali Tukai, ametoa shukurani hizo wakati akitoa taarifa ya Utendaji, Mafanikio na Mwelekeo wa MSD, kwenye Mkutano baina ya taasisi hiyo na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, uliofanyika kwa Uratibu wa Msajili wa Hazina (TR), Septemba 28, 2023, katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.

Amesema, kutokana Rais Dk. Samia, kuipatia MSD fedha za kutosha tena kwa wakati, taasisi hiyo imeweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo, kiasi kwamba hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya katika Bohari Kuu ya Dawa, imeongezeka kutoka asilimia 51 mwezi Juni 2022 hadi kufikia asilimia 64 Juni 2023.

Tukai amesema, katika mwaka wa fedha 2022/23 MSD imepokea Sh. bilioni 190.3 ambazo ni nyingi zaidi ikilinganishwa na Sh. bilioni 134.9 ilizopokea mwaka wa fedha 2021/22, sawa na asilimia 95, na kukiri kwamba kiwango cha fedha zilizotolewa 2022/2023 hakijawahi kutokea katika historia ya MSD.

Kuhusu usambazaji wa bidhaa, Mkurugenzi Mkuu Tuvai, akasema, MSD imeimarisha mfumo wa usambazaji kwa kusambaza bidhaa za afya mara 6 kwa mwaka, kila baada ya miezi miwili kwa mwaka wa fedha 2022/23 badala ya mara 4 kwa mwaka miezi mitatu, hivyo kupunguza muda wa vituo vya afya kusubiri bidhaa za afya.

Tuvai alisema, MSD imenunua matrela 16 yenye thamani ya Sh. bilioni 2.6 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa za afya kwa asilimia 16, na inatumia mifumo shirikishi ya TEHAMA (PoD) ili kuhakikisha bidhaa za afya zinapokelewa kielekroniki katika vituo vya kutolea huduma za afya na pia kuimarisha ufuatiliaji wa magari kwa kutumia mifumo.

Akizungumzia mafanikio ya taasisi hiyo, Tuvai amesema katika neo la uzalishaji bidhaa, MSD imekamilisha Ujenzi wa Kiwanda cha mipira ya mikono “gloves”  cha 'Mikokono Gloves', kilichopo Idofi, mkoani Njombe, pia MSD imehusisha sekta binafsi kutambua maeneo ya uwekezaji ya bidhaa za afya za kimkakati kama za vidonge (tablets), rangi mbili (capsules), vimiminika na bidhaa zitokanazo na zao la pamba.

Tuvai alisema, pia MSD ipo katika kukamilisha taratibu za usajili na uendeshaji Kiwanda cha barakoa cha N95 kilichopo Keko jijini Dar es Salaam, akisema uzalishaji wake utakidhi mahitaji ya bidhaa hiyo nchini, halikadhalika kuanzisha kampuni tanzu “MSD Medipharma Manufacturing Company Ltd” itakayosimamia uzalishaji wa bidhaa za afya.

"MSD pia imefanya maboresho mbalimbali ambapo hadi sasa imeweza kuimarisha mifumo ya usimamizi kwenye ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya, Kuimarisha ushirikiano na wadau wa mnyororo wa ugavi, Kushirikisha balozi zetu zilizopo China, Algeria, Urusi na Korea ya Kusini na kutafuta wadau wa uzalishaji na ununuzi", akasema Tuvai.

Alisema hatua nyingine za MSD kusonga mbele ni kutumia wadau wa ndani na nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa bidhaa za afya nchini, Kuboresha mifumo simamizi kwa kutumia TEHAMA mfano; mfumo wa usimamizi wa magari, kuanzisha kampuni tanzu ili kuweza kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya kwa ufanisi, ugatuzi wa utendaji kutoka Makao Makuu kwenda Ofisi za Kanda.

Tuvai alisema MSD ina ofisi zipatazo kumi za kanda zikiwemo za Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Kagera, Mtwara na Dodoma.” Alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Ali Tukai, akitoa taarifa ya Utendaji, Mafanikio na Mwelekeo wa MSD, kwenye Mkutano baina ya taasisi hiyo na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, uliofanyika kwa Uratibu wa Msajili wa Hazina (TR), Septemba 28, 2023, katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam. Walioketi, kutoka kushoto ni Meneja Uhusuano MSD Etty Kusiluka, Meneja Mipango Ufuatiliaji na Tathmini MSD  Hassan Ally, Mkuu wa Ktengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), Eric Mkuti na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile.

Afisa Uhusiano Mwnadamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akitoa mwongozo wa Mkutano huo.
Meza Kuu wakiwa wamesimama kupokea dua iliyokuwa ikifanywa mwanzoni mwa Mkutano huo.
Washiriki wa kikao hicho wakiwa wamesimama kupokea dua mwanzoni mwa Mkutano huo.
Meneja Uhusuano MSD Etty Kusiluka, akizungumza mwanzoni mwa Mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Ali Tukai (kushoto), akijadiliana jambo na Mkuu wa Ktengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), Eric Mkuti na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile (kulia), wakati wa Mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Ali Tukai, akitoa taarifa ya Utendaji, Mafanikio na Mwelekeo wa MSD, kwenye Mkutano huo.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo.
Mhariri wa habari wa Gazeti la Serikali la Habari Leo Mgaya Kingoba, akiuliza maswali wakati wa Mkutano huo. Wajumbe mbalimbali walipata nafasi ya kuuliza maswali.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Ali Tukai, akijibu maswali.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa kweye Mkutano huo. Mbele ni Joe Nakajumo, Yasin Sadik, Joseph Kulangwa.
Mkuu wa Ktengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), Eric Mkuti akijadili jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile mwishoni mwa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akitoa hotuba ya shukurani mwishoni mwa mkutano huo.

 

TAARIFA KAMILI YA MSD ILIYOWASILISHWA NA MKURUGENZI MKUU TUKAI👇


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages