LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 18, 2023

MBUNGE LUGANGIRA AMUOKOA BABA LISHE ALIYEIBIWA VIFAA MGAHAWANI



MBUNGE wa Viti Maalumu, Neema Lugangira ametoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa Baba Lishe mwenye uhitaji maalumu, Mzee Novat Kaijage 

Ametoa vifaa hivyo baada ya Baba Lishe huyo kumpatia taarifa Mbunge Lugangirta kuwa ameibiwa vifaa vyake vyote katika mgahawa wake.

Jumapili 17/9/2023, Mhe Lugangira alipata fursa akaongea na Mzee Novat Kaijage ambapo alimwambia ameibiwa vitu katika Mgahawa wake hivyo anaomba msaada wa kununuliwa vitu vilivyoibiwa na pia aliomba Mtungi wa Gesi. 

Kwa kumuonea huruma, ndipoSeptemba 18, 2023  Lugangira alichukua uamuzi wa kumtuma katibu wake wa ubunge,Mansoor Amri, kwenda kwenye Mgahawa wa Mzee Novat Mwijage uliopo Bukoba Mjini na kumkabidhi vitu vyote alivyohitaji.

Hivi karibuni mbunge huyo aliendesha kampeni ya Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira. ambapo aligawa majiko ya gesi kwa wanawake.




Leo 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages