Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kama Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Inayojishughulisha na Elimu Duniani (Global Partnership for Education), amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Jijini New York, Marekani.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala ya elimu, hasa kuelekea Mwaka wa Elimu wa Afrika, 2024.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇