LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 20, 2023

SHULE YA AWALI YAJENGWA LUMUMBA

NDUGU Selina Koka ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na ndugu Silyvestry Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini wanajenga shule ya awali ambayo ni ya Jumuiya ya Wazazi tawi la Lumumba Kata ya Pangani.


Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge, viongozi hao wameamua kujenga shule hiyo kama muendelezo wa jitihada zao za kuinua sekta ya Elimu Kibaha pamoja na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ikumbukwe kuwa  Jumuiya ya Wazazi kwa mujibu wa kanuni yake, imepewa dhamana ya kusimamia mambo yanayohusu elimu, Mazingira na Malezi.


Ni imani ya viongozi hao kuwa shule hiyo itakapokamilia itatoa fursa ya elimu na malezi kwa watoto wetu wa Tawi la Lumumba na matawi ya jirani.


Ujenzi wa Shule hyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Mwaka huu ili mapema mwakani watoto waanze kusoma.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages