LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 18, 2023

REA KUKOPESHA WANANCHI UJENZI WA VITUO VIDOGO VYA MAFUTA VIJIJINI

 


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala hiyo na mwelekeo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Agosti 18, 2023 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

 
Na Richard Mwaikenda, Dodoma

SERIKALI kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA),imetangaza kuanza usambazaji wa vituo vidogo vya mafuta vijijini.

Mpango huo umebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy wakati wa mkutano na vyombo vya habari jijini Dodoma Agosti 18, 2023.

Amesema usambazaji wa Mradi huo unahusu kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kusambaza bidhaa za mafuta katika maeneo mbalimbali ya vijijini.  


Ametaja utaratibu utakaofuatwa pamoja malengo kuwa ni;


Mradi wa utoaji Mikopo ya Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya mafuta ya Petroli na Diseli vijijini Tanzania bara;

Malengo Makuu ikiwa ni:

Kulinda Mazingira na Afya ya Watumiaji na Kuboresha upatikanaji na Usambazaji wa Mafuta vijijini.

Kiasi cha Mwisho cha Mkopo ni TZS 75,000,000;

Kiasi cha Riba ni 5%;

Muda wa Marejesho ni Miaka 7;

Kwa mwaka 2023/24 kiasi cha TZS bilioni 10 kimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa waendelezaji;

Kwasasa, Wakala unaendelea kupokea Maombi ya Waombaji;

Mwisho wa Kupokea Maombi ni 25 Agosti 2023.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages